IQNA

Jinai za Israel

Mpalestina afariki mwezi mmoja baada ya kupigwa risasi na askari katili wa Israel

21:01 - August 27, 2023
Habari ID: 3477504
AL-QUDS (IQNA) - Mpalestina aliyekuwa na umri wa miaka 20 amefariki dunia kutokana na majeraha mwezi mmoja baada ya kupigwa risasi na askari katili wa utawala haramu wa Israel waliokuwa wakishamulia eneo moja la Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

Shirika la habari la Palestina, WAFA lilisema siku ya Jumamosi kwamba Ezzedin Kanan, alipigwa risasi ya kichwani Julai 3 wakati wa moja ya hujuma kali za kijeshi za Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

Mwili wa Ezzedine, ambaye alitoka mji wa Jaba' kusini mwa Jenin, ulizikwa Jumamosi baada ya Sala ya adhuhuri.

Israel ilianzisha mashambulizi ya anga na ardhini kwenye kambi ya wakimbizi ya Jenin mapema Julai.

Uvamizi huo, ambao ulikuwa mkali zaidi katika Ukingo wa Magharibi katika miongo miwili, ulisababisha vifo vya raia 13, wakiwemo watoto watano. Zaidi ya wengine 140 walijeruhiwa, 30 kati yao vibaya.

Kwa kisingizio cha kuwasaka Wapalestina "wanaotafutwa", wanajeshi wa Israel mara kwa mara huvamia miji mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi, na hivyo kuzua mapigano makali na wakaazi.

Uchokozi wa kinyama wa utawala huo umesababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina 200 katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Ghaza mwaka huu. Wengi wa majeruhi hawa wametokea katika Ukingo wa Magharibi.

Habari zinazohusiana
captcha