IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Kongamano la Kuukaribisha Mwezi wa Ramadhani London

21:12 - February 25, 2023
Habari ID: 3476623
TEHRAN (IQNA)- Jumba la Makumbusho ya Victoria na Albert la London limeaandaa mkutano kwa mnasaba wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa tovuti ya Event Brite, mkutano huu utafanyika kwa jina la "Welcome Ramadan Conference" yaani Kongamano la Kuukarisbisha Mwezi wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa waandalizi, kongamano hilo linafanyika kwa lengo la kuandaa jumuiya ya Waislamu wa Uingereza kwa ajili ya ujio wa Ramadhani, mwezi mtukufu zaidi katika kalenda ya Kiislamu  ambao pia ni mwezi wa Saumu.

Kongamano hilo ni ni sehemu ya Ramadhan Tent Project au Mradi wa Hema ya Ramadhani.

Mradi wa Hema ya Ramadhani, uliozinduliwa kwa mara ya kwanza London, ulipata umashuhuri wa kimataifa mwaka wa 2011 wakati kikundi cha wanafunzi kutoka London School of Oriental and African Studies (SOAS) kilipoweka hema ndogo katika bustani ya chuo kikuu na kuwaalika wapita njia kujumuika nao wakati wa futari.

Ujumbe wa waandaaji wa mkutano huu unasema: “Tuna hamu ya kuwaleta pamoja wanazuoni, wanaharakati, mashirika ya kijamii, mashirika ya misaada na umma kwa ujumla na kusherehekea mwezi huu wenye baraka katika mfululizo wa meza za duara zinazojadili umuhimu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa Waislamu."

Hivi sasa, mradi huu sasa unafanyika London, Manchester, Plymouth, Ndola, Toronto, Portland na Istanbul na umekuwa shirika rasmi lisilo la faida na unapanga kupanua shughuli zake katika siku zijazo.

Kongamano hilo  la kukaribisha Ramadhani litafanyika Jumapili, Machi 5.

4124268

Kishikizo: ramadhani london SOAS
captcha