IQNA

Sera za Kigeni

Iran yataka jamii ya kimataifa ikabiliane na chuki dhidi ya Uislamu

18:26 - March 16, 2023
Habari ID: 3476716
TEHRAN (IQNA)- Ofisi ya Uwakilishi wa Kudumu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mashirika ya kimataifa yaliyo na makao makuu yao mjini New York Marekani, imeandika kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya kupambana na Chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) kwamba: "Iran inasisitiza mshikamano wake kamili na wahanga wa mashambulio yanayochochewa na chuki dhidi ya Uislamu kote duniani."

Katika miaka ya hivi karibuni, serikali za Magharibi zimekuwa zikiunga mkono watu waovu wanaopinga Uislamu, ambao wanatusi na kuzivunjia heshima hadharani thamani za Uislamu na Waislamu. Tarehe Machi 15 imetengwa na Umoja wa Mataifa kama Siku ya Kupambana na chuki dhidi ya Uislamu kupitia azimio la umoja huo lililopitishwa mwaka 2022.

Ofisi ya Uwakilishi wa Kudumu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mashirika ya kimataifa yaliyoko mjini New York imeandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Chuki dhidi ya Uislamu kwamba: "Wakati umefika kwa jamii ya kimataifa kupambana na maneno na vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu ambao wanaunda sehemu kubwa na muhimu ya jamii ya mwanadamu."

Ofisi hiyo ya Iran imeongeza kuwa: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inavichukulia vitendo vyote vya ukatili dhidi ya dini au imani kuwa ni vya kusikitisha mno na inasisitiza mshikamano wake kamili na wahanga wa mashambulizi yanayochochewa na chuki dhidi ya Uislamu kote duniani."

Ofisi ya Uwakilishi wa Kudumu ya Iran mjini New York imeongeza kuwa: "Katika miongo michache iliyopita, mtandao mpana wa vyombo vya habari vinavyopinga Uislamu umeibuka; ambapo vinaeneza na kuchochea mazingira ya chuki na matusi dhidi ya Waislamu, jambo ambalo bila shaka ni tishio kwa suala zima la haki za binadamu."

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran

Juzi pia Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba: Wale wenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu hawaamini maadili yoyote ya kibinadamu na dini za Mwenyezi Mungu.

Serikali za nchi za Magharibi katika miaka ya karibuni zimewaunga mkono na kuwafadhili watu wanaoneza chuki dhidi ya Uislamu ambao wamezivunjia heshima thamani na matukufu ya dini tukufu ya Uislamu na Waislamu. 

Kwa sababu hiyo Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka jana lilipasisha azimio likiitangaza tarehe 15 mwezi Machi kila mwaka kama Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Chuki dhidi ya Uislamu. 

Nasser Kan'ani Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametwiti leo kwa kuandika kuwa: "Dini Tukufu ya Uislamu na Mtume wa rehma, Muhammad (S.A.W) alibeba ujumbe wa amani, urafiki na kuishi pamoja kkwa maani wanaadamu wote. 

Kan'ani aliongeza kuwa: Wale wanaoeneza chuki dhidi ya Waislamu na Uislamu hawaamini thamani na maadili yoyote ya kibinadamu na ya dini za mbinguni bali wanaamini kuwa maslahi yao haramu yamo katika kueneza hitilafu na mifarakano kati ya matabaka mbalimbali ya wanaadamu. 

3482837

captcha