IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Waislamu waingia na hofu baada ya Msikiti kuhujumiwa huko Cambridge, Kanada

22:58 - March 03, 2023
Habari ID: 3476653
TEHRAN (IQNA) – Jumuiya ya Waislamu katika eneo la Cambridge nchini Kanada (Canada) wanasema wameingiwa na hofu tangu msikiti wao ulipohujumiwa na kuharibiwa wiki iliyopita.

Asubuhi ya Februari 22, washiriki wa Masjid wa Hespeler walifika kwenye msikiti huo ulio barabra ya Winston Boulevard na kugundua mahali pao pa ibada pameharibiwa, na kuwaacha wengi wakiwa na wasiwasi na woga.

Jiwe lilikuwa limerushwa kupitia dirisha la ghorofa ya chini, ambapo mwenyekiti wa kamati ya msikiti huo, Waqas Bhutta alisema kitendo hicho kilikuwa na motisha ya chuki.

Huku polisi wakiendeleza uchunguzi kwa lengo la kuwakamata waliohusika na uhalifu huo, Waislamu wa eneo hilo  sasa wanasema inabidi wawe macho zaidi.

Msikiti umeanza kupendekeza kwamba watu wanaotoka Msikitini wasafiri kwa vikundi na waepuke kutoka peke yao.

Hata kama shambulio hilo halikuchochewa na chuki, kitendo tu cha kulengwa kinaongeza hofu kwa kiwango kikubwa, alisema Sarah Shafiq, mkurugenzi mtendaji wa Muungano wa Wanawake wa Kiislamu wa KW(CMW-KW).

Kulingana na muungano huo, chuki dhidi ya Uislamu imekuwa ikiongezeka katika eneo hilo.

"Kumekuwa na ripoti mbili katika jiji la Kitchener mwezi Februari ambapo hijabu za wanawake wa Kiislamu zilitolewa. Huu ni uhalifu wa chuki," alisema.

Wanawake wa Kiislamu wanalengwa mara kwa mara, haswa ikiwa wamevaa kitambaa kichwani.

Kwa msingi huo mwenyekiti wa kamati ya Hespeler Masjid amependekeza wanawake kuondoka msikitini kukaa katika kundi.

"Ni asilimia 25 tu ya uhalifu huu wa chuki unaoripotiwa na jamii na ni asilimia moja tu ambao huchunguzwa na polisi," alisema Shafiq. "Watu hawana imani kuwa wakiripoti hatua zitachukuliwa, hivyo wanakaa kimya."

3482684

captcha