IQNA

Uhalifu

Watu wafariki baada ya kudungwa kisu katika Kituo cha Waislamu Ureno

17:24 - March 29, 2023
Habari ID: 3476781
TEHRAN (IQNA) - Watu wawili wameuawa katika shambulio la kudunga visu kwenye Kituo cha Waislamu cha Ismaili katika jiji kuu wa Ureno, Lisbon.

Waziri Mkuu wa Ureno Antonio Costa aliwaambia waandishi wa habari kuwa ni "kitendo cha uhalifu" na kwamba watu wawili wamepoteza maisha katika tukio hilo.

Polisi walimpiga risasi mshukiwa ambaye sasa amelazwa hospitalini, Costa alisema.

"Kila kitu kinaashiria kuwa tukio lililotekelezwa na mtu moja," Costa alisema, bila kufafanua. Polisi hawakutoa maoni yoyote mara moja baada ya tukio hilo la Jumanne lakini walisema watatoa habari zaidi baadaye.

Hakukuwa na taarifa za haraka juu ya utambulisho wa waliouawa.

Polisi wenye silaha kutoka kitengo maalum cha operesheni walionekana nje ya jengo hilo. Costa alisema polisi wanachunguza shambulio hilo na ilikuwa mapema sana kutafakari juu ya nia.

Baadhi ya duru zinasema mshambuliaji huyo ni mkimbizo kutoka Afghanistan na kwamba binti zake watatu walihudhuria masomo ya Kireno katika kituo hicho.

Waislamu wa Shia Imami Ismaili, wanaojulikana kwa ujumla kama Ismailia, ni wa tawi la Uislamu la Shia, kulingana na tovuti yao. Waislamu wa Ismailia wanaoishi katika zaidi ya nchi 25 duniani kote.

Ureno haijarekodi mashambulizi yoyote makubwa ya kigaidi katika miongo ya hivi karibuni, na vurugu za kidini hazijasikika.

3482970

Kishikizo: ismaili waislamu ureno
captcha