Swala hiyo iliongozwa na Sheikh Abdul Mahdi al-Karbalayi, msimamizi wa haram hiyo na mwakilishi wa marjaa mkuu wa Kishia nchini Iraq. Baada ya swala, Sheikh Muhammad Ali Muhammad Al-Ghurairi, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Masheikh wa Kiislamu Iraq, amesema: “Tuko kaktika haram takatifu za Imamu Hussein (AS) na Hazrat Abbas (AS). Sisi ni wana wa nchi hii, na tunaamini urithi wetu na asili yetu huanzia hapa , katika eneo hili takatifu na uwepo wa bwana wangu Imamu Hussein (AS).”
Sheikh huyo wa Kisunni aliendelea: “Tumekuja kutoa rambirambi zetu katika siku ya mwisho ya Muharram. Kama Wairaqi, tunaponya majeraha yetu sambamba na baba wa mashahidi, Imamu Hussein (AS) na ndugu yake Abu al-Fadl al-Abbas (AS). Leo tunapeleka ujumbe kwa wanaotutusi kwamba sisi ni taifa moja , lililoungana na kusimama kwa pamoja.”
Alisisitiza kuwa: “Viongozi wetu wa kidini ni bendera za taifa hili – kwa hakika, bendera za taifa lake – na daima wamekuwa na juhudi za kuunganisha safu. Bila uwepo wa viongozi hawa, tusingefikia kiwango hiki cha usalama, afya, mapenzi na udugu.”
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Sheikh Al-Ghurairi alisema: “Wairaqi daima wamekuwa pamoja na Palestina na Gaza – walikuwa na bado ni watetezi wa haki za Wapalestina. Viongozi wetu wa kidini na masheikh wamekwisha tangaza hadharani kuwa wanaunga mkono Palestina.”
Akalaani vikali utawala wa Kizayuni kwa kuzingira watu milioni mbili na kuwanyima chakula, akisema kuwa sasa watoto wa Gaza wanakufa kwa njaa. “Tunaiga azma hii kutoka kwa viongozi wetu wa kiroho, na hata kutoka kwa mapinduzi ya Hussein (AS). Tunajifunza dhamira thabiti kwamba kuwasaidia wanyonge ni jukumu la kila mtu mwenye uwezo – hata kwa neno au mchango mdogo. Hili ndilo tumaini letu – kwamba Mwenyezi Mungu atauondoa msiba huu kutoka Gaza, Iraq na nchi zote za Waislamu, ili Waislamu duniani kote wafurahie usalama na utulivu kupitia baraka za siku hizi tukufu za mwezi wa Muharram.”
3494013