IQNA

Mufti wa Al-Quds azuiwa kuingia Msikiti wa Al-Aqsa baada ya hotuba kuhusu njaa Gaza

17:58 - July 28, 2025
Habari ID: 3481015
IQNA-Sheikh Muhammad Ahmad Hussein, Mufti Mkuu wa Al-Quds, amepigwa marufuku na utawala dhalimu wa Israel kuingia Msikiti wa Al-Aqsa ulio mjini Quds (Jerusalem) kwa muda wa wiki moja, marufuku ambayo inaweza kuongezwa

Hatua hii imechukuliwa baada ya hotuba yake ya Ijumaa iliyolaani vikali mateso na njaa inayoendelea Gaza, ambako zaidi ya watu 59,000 wameuawa katika mashambulizi ya utawala dhalimu wa Israel tangu Oktoba 2023, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

Katika hotuba hiyo, Mufti alisema: "“Waislamu, enyi watu wa Isra na Mi’raj, ubinadamu leo unakandamizwa na dhulma... Wengine wananyimwa chakula na wanakufa kwa njaa mbele ya macho ya dunia inayodai kutetea haki za binadamu, madai ambayo uhalisia unayakanusha.”

Mufti amesema  aliitwa na ujasusi wa Israeli kwa mahojiano kabla ya kupokea amri ya marufuku. Alisisitiza kuwa hotuba yake ilikuwa ni wajibu wa kidini na kimaadili wa kukemea dhulma.

Ukandamizaji unaoendelea Gaza umepelekea maafa ya kibinadamu yasiyo na mfano wa karibuni. Takriban watoto 100,000, wakiwemo watoto wachanga 40,000, wanakabiliwa na njaa kali, huku mashirika ya misaada yakionya kuwa chakula cha tiba kinakaribia kuisha.

Maafisa wa utoaji misaada katika Ukanda wa Gaza wametangaza leo kuwa watu 127 wamekufa shahidi kwa utapiamlo na njaa kutokana na mzingiro mkubwa lililowekewa eneo hilo na utawala wa kizayuni na hatua ya utawala huo ghasibu ya kuzuia uingizaji misaada ya kibinadamu.

Bassam Zaqout, mkurugenzi wa misaada ya kitiba katika Ukanda wa Ghaza, ameiambia televisheni ya Al Jazeera kwamba, watu 127 wamepoteza maisha kutokana na lisheduni katika Ukanda wa Gaza.

Zaqout ameongezea kwa kusema, inapasa vivuko salama vianzishwe kwa ajili ya kuingizwa misaada ya kitiba na ya kibinadamu katika Ukanda wa Ghaza na vita lazima vikomeshwe.

Mkurugenzi huyo wa misaada ya kitibau huko Ghaza ametahadharisha kwa kusema: "tuna wagonjwa 12,000 wanaohitaji upasuaji wa haraka na tunatala wapelekwe nje ya Ukanda wa Ghaza kwa matibabu. Kutokana na uhaba wa mara kwa mara wa chakula na dawa kuna tatizo la kuponya majeraha ya majeruhi, na tunapokea zaidi ya majeruhi 450 kila siku".

Zaqout amebainisha kwa kusema: "tuna matatizo makubwa kutokana na uhaba wa mafuta, na kwa sababu hii tunakaribia kusimamisha huduma zetu".

3494023

Habari zinazohusiana
Kishikizo: gaza njaa israel mufti quds
captcha