IQNA

Waombolezaji wa Bani Amer waingia Karbala kabla ya Arbaeen

17:52 - July 28, 2025
Habari ID: 3481014
IQNA-Kundi la maombolezo la Bani Amer, mojawapo ya makundi makubwa zaidi ya waombolezaji nchini Iraq, limeanza matembezi yake ya kiroho kutoka Basra kuelekea Karbala, likiwa limevalia mavazi meupe ya kitamaduni, kwa ajili Arbaeen ya mwaka huu.

Safari hii ya kila mwaka huanza wiki kadhaa kabla ya Arbaeen, na huhitimishwa tarehe 19 Safar, siku moja kabla ya siku rasmi ya Arbaeen, kwa kuwasili kwao katika kaburi takatifu la Imam Hussein (AS) huko Karbala.

Katika eneo la Bain-ul-Haramain, kati ya makaburi ya Imam Hussein (AS) na Hadhat Abbas (AS), kundi hili huimba kauli mbiu za kidini na aya za Qur’ani kwa sauti ya huzuni na matumaini. Arbaeen yenyewe ni kumbukumbu ya siku ya 40 baada ya Ashura, siku ya kuuawa kwa mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), Imam Hussein (AS), katika vita vya Karbala mwaka 61 Hijria sawa 680 Miladia.

Ziyara ya matembezi ya Arbaeen ni mojawapo ya mikusanyiko mikubwa zaidi ya kidini duniani, ikikusanya mamilioni ya Waislamu wa madhehebu ya Shia, pamoja na baadhi ya Sunni na wafuasi wa dini nyingine, wakitembea kwa miguu kutoka miji mbalimbali hadi Karbala. Mwaka huu, Arbaeen itaadhimishwa tarehe 14 Agosti 2025.

3494022

captcha