Ayatullah Khamenei alitoa kauli hiyo siku ya Jumanne katika hafla iliyofanyika katika Hussainiya ya Imam Khomeini mjini Tehran, ikiwa ni kumbukumbu ya siku ya arobaini tangu mashahidi wa vita hiyo walipopoteza maisha. Hafla hiyo ilihudhuriwa na familia za mashahidi, viongozi wa serikali, pamoja na wananchi kutoka nyanja mbalimbali.
Amesema kuwa vita hiyo vilikuwa fursa kwa Jamhuri ya Kiislamu kuonesha uthabiti wake na uwezo wake wa kiistratijia, huku akisisitiza kuwa chanzo kikuu cha uadui dhidi ya Iran ni “imani, elimu, na umoja wa taifa.”
“Ubeberu wa Kimataifa, unaoongozwa na Marekani, unapingana na dini yenu na maarifa yenu,” alisema Ayatullah Khamenei. “Wanapinga imani hii ya kina ya watu wetu, wanapinga umoja wao chini ya bendera ya Uislamu na Qur’ani, na wanapinga elimu yenu.”
Kauli hizi za Kiongozi zinakuja baada ya hujuma ya tarehe 13 Juni iliyoendeshwa na Israel dhidi ya maafisa wa ngazi ya juu wa Iran na wanasayansi wa nyuklia, tukio la kigaidi lililosababisha vifo vya raia wengi wasio na hatia. Siku chache baadaye, Marekani iliongeza chachu ya vita hiyo kwa kushambulia kwa mabomu vituo vitatu vya nyuklia vya kiraia nchini Iran.
Katika hatua ya kujibu kwa nguvu, Vikosi vya Ulinzi vya Iran vilitekeleza mashambulizi ya kisasi dhidi ya malengo ya kimkakati ndani ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) na pia vikashambulia kambi ya kijeshi ya al-Udeid ya Marekani iliyoko huko Qatar ambayo kituo kikubwa zaidi cha kijeshi cha Marekani katika eneo la Asia ya Magharibi.
Operesheni hizo za pamoja za Iran ziliwalazimu wavamizi kusitisha mashambulizi kufikia tarehe 24 Juni.
Ayatullah Khamenei alikanusha madai ya Magharibi kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na masuala ya haki za binadamu, akisema madai hayo ni kisingizio tu; hoja ya msingi ya maadui ni nguvu inayozidi kuongezeka ya Jamhuri ya Kiislamu.
Soma Zaidi:
“Ata kwa neema ya Mwenyezi Mungu, taifa letu halitaiacha dini yake wala elimu yake,” alisema. “Tutadumu kuchukua hatua madhubuti katika kuimarisha imani yetu na kuendeleza maendeleo ya kisayansi kwa kina.”
Kiongozi Muadhamu aliongeza, “Kwa masikitiko ya maadui wetu, tutaweza kuifikisha Iran kwenye kilele cha maendeleo na fahari.”
3494053