
Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 103 ya Surah Al Imran: “Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka".
Maana ya aya ya “kamba ya Mwenyezi Mungu” ni kila fikra inayotuunganisha na Mwenyezi Mungu yaani Uislamu, Qur'ani Tukufu, Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) na Ahl-ul-Bayt wake au watu wa nyumba yake (AS).
Aya hii inaashiria neema kubwa ya umoja na udugu na inawataka Waislamu kutafakari juu ya hali ya kusikitisha ya huko nyuma na kulinganisha mifarakano iliyotangulia na umoja uliopatikana
Aidha ayah ii inaashiria kuzikurubisha nyoyo za waumini kwa Mwenyezi Mungu, na kusema: “Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Hii inaweza kutajwa kama moja ya miujiza ya Uislamu ambayo ilieneza urafiki miongoni mwa Waarabu wakati walipokuwa katika uhasama na vita kabla ya ujio wa Uislamu.
Mambo Muhimu kutoka katika Aya ya 103 ya Surah Al Imran
Kuunda umoja kati ya mioyo inawezekana tu kwa taufiki yake Mwenyezi Mungu. Katika Aya ya 63 ya Surah Al-Anfal, Mwenyezi Mungu anamwambia Mtukufu Mtume (SAW): “… Na akaziunga nyoyo zao. Na lau wewe ungeli toa vyote viliomo duniani usingeli weza kuziunga nyoyo zao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye waunganisha. Hakika Yeye ndiye Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima.”
Mfarakano na migawanyiko ni miongoni mwa adhabu za Mwenyezi Mungu. Nukta nyingine ni kuwa katika Uislamu kutosema ukweli kwa madhumuni ya kuleta umoja inajuzu na kusema ukweli unaoweza kusababisha mfarakano ni Haramu.
Nukta muhimu tunazojifunza: