IQNA

IQNA yazindua Kitajiki kama lugha yake ya 22

12:26 - May 14, 2023
Habari ID: 3476994
TEHRAN (IQNA) – Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA)  limeongeza lugha ya Tajiki ambayo itakuwa lugha ya 22 kwenye shirika hilo la habari.

Sherehe za ufunguzi zmefanyika Jumapili kwa kuhudhuriwa na Hujjatul Islam Mohsen Qomi, mkuu wa masuala ya kimataifa wa Ofisi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa  ni shirika la kwanza la habari nchini Iran kuwa na lugha 22 na inalenga kuongeza usamabzwaji wa habari za Qur'ani kimataifa. Hivi sasa, kurasa za lugha za kigeni zina watembeleaji wengi kuliko ukurasa wa Kifarsi au Kiajemi.
Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa linaamini kwamba habari zinazohusiana na Qur'ani Tukufu zinaweza kuwa na nafasi ya kuunganisha mataifa ya Kiislamu na Waislamu wa dunia, kama ambavyo  Qur'ani yenyewe inawaleta pamoja Waislamu.
Uzinduzi wa lugha za IQNA hutokana na tafiti zilizofanywa na chombo hiki cha habari pamoja na maoni kutoka kwa watumiaji na taasisi za Kiislamu katika nchi nyinginezo.
Kitajiki ni lugha rasmi ya Tajikistan na pia inazungumzwa katika sehemu za Uzbekistan, Kyrgyzstan na Afghanistan. Kulingana na Britannica, Kitajiki kinazungumzwa na zaidi ya watu milioni 7 walioenea kote Tajikistan na Asia ya Kati. Tajiki inatajwa kuwa moja ya lahaja za Kiajemi na kwa hiyo inahusiana na lugha nyinginezo katika familia ya lugha ya Kiajemi kama vile Kiajemi, Kidari na Kipashto.

IQNA Opens Tajiki as Its 22nd Language
Kitajiki cha Tajikistan kimetofautiana kutoka kwa Kiajemi kama inavyozungumzwa nchini Afghanistan na Iran kwa sababu ya mipaka ya kisiasa, kutengwa kwa kijiografia, mchakato wa kusanifisha na ushawishi wa Kirusi na lugha jirani za Kituruki.
Watajiki waliowengi  ni Waislamu wa Kisunni wa madhehebu ya Hanafi, lakini pia kuna baadhi ya Watajiki ni Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaofuata Maimamu Kumi na Wawili na wengine ni Ismailia. Wanaishi kwa amani na makabila na dini zingine katika maeneo kama Badakhshan, Herat, Balkh, nk.

3483554

captcha