IQNA

Mawaidha

Adhabu ya kudumu kwa makafiri huko Akhera

21:10 - May 14, 2023
Habari ID: 3477000
TEHRAN (IQNA) – Suala la adhabu ya kudumu kwa makafiri huko Akhera limekuwa mada kuu ya mjadala miongoni mwa wanachuoni wa Kiislamu, hususan kwa kuzingatia rehema za Mwenyezi Mungu.

Katika Surah Al-Fatiha, sura ya kwanza ya Qur'ani Tukufu, tunasoma kuhusu Mwenyezi Mungu kuwa Rahman na Rahim yaani Mwingi wa Rehema na Mwingi wa Kurehemu na kwamba rehema yake ni kwa viumbe vyote. Basi vipi mtu anaweza kuhalalisha kudumu kwa adhabu kwa baadhi ya makafiri huko Akhera?

Wengine wanarejelea nia ya makafiri, wakisema kwa sababu walikuwa na nia ya kuendelea kufanya dhambi hapa duniani, adhabu yao huko akhera nayo itadumu. Lakini adhabu kwa kutegemea nia pekee haikubaliki kwa mujibu wa Sharia.

Baadhi ya wengine wanasema kwamba Khulud (kuwa mahali pa kudumu) motoni ina maana ya kubaki humo kwa muda mrefu na hilo linakubalika kutokana na kwamba baadhi ya dhambi kama vile Kufr ni mbaya sana. Lakini hili pia haliendani na kanuni za Fiqh.

Wengine, wakati huo huo, wanasema kudumu kwa adhabu kunatokana na maamuzi ya Mwenyezi Mungu, yaani, adhabu hudumu kwa kadri Mungu anataka.

Katika tafsiri ya Qur'ani Tukufu, kanuni moja kuu ni kwamba Mwenyezi Mungu si dhalimu na nyingine ni kwamba mfumo wa ulimwengu umeegemezwa juu ya sheria ya sababu na athari. Kudumu kwa adhabu inapaswa kueleweka kwa kuzingatia haya mawili.

Sasa je, dhambi kama Kufr inaongoza kwenye adhabu ya kudumu na italingana na Mungu kuwa Adil (mwadilifu)? Jambo moja la kukumbuka ni kwamba ufahamu wetu wa Khulud unatokana na ufahamu wetu wa sasa na sisi ni viumbe ambao tuko chini ya mipaka ya wakati. Lakini huko akhera tutakuwa chini ya mipaka hii tena?

Ikiwa sivyo, basi sisi katika hali ya sasa hatuwezi kuwa na ufahamu sahihi na kamili wa hali za wakati huo.

Kwa hivyo, ingawa suala la kuadibu kwa kudumu linaweza kuwa haliendani na Mwenyezi Mungu kuwa Rahman na Rahim, tunapaswa kujaribu kulielewa ndani ya mfumo wa sheria ya sababu na matokeo na ukweli kwamba Mungu si dhalimu.

captcha