IQNA

Hija 1444

Saudi Arabia yafanya mazoezi ya usalama mtandaoni kabla ya Hija

16:48 - June 02, 2023
Habari ID: 3477082
TEHRAN (IQNA) – Mazoezi ya usalama wa mtandao wa intaneti kwa ajili ya ibada ya Hija ya mwezi ujao yamefanyika nchini Saudi Arabia.

Mazoezi hayo yamelenga kuboresha huduma kwa Mahujaji na kuzuia vitisho vya mtandao vinavyoweza kutokea.

Mazoezi hayo, yaliyozinduliwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Usalama wa Mtandao (NCA), yalishirikisha zaidi ya mashirika 100 ya Saudi yakiwakilishwa na maafisa 350 wa usalama wa mtandao.

Hafla hiyo ya siku mbili ambayo iliyozinduliwa katika mji wa Bahari Nyekundu wa Saudia wa Jeddah ilikuwa sehemu ya msaada wa NCA kwa taasisi za kitaifa kufanya kazi za usalama wa mtandao wakati wa msimu wa Hijja na ililenga kujumuisha ustahimilivu wao dhidi ya vitisho vinavyoweza kutokea na kukuza usalama wa wataalam, wakala wa serikali umesema. .

"Mazoezi hayo yalijumuisha seti ya shughuli za kiufundi na kiutawala na iliangazia uigaji wa aina tofauti za mashambulizi ya mtandaoni pamoja na kutumia mbinu ya kukabiliana na ajali za dharura za mtandao," NCA iliongeza katika taarifa.

Tukio hilo pia lililenga kuboresha utayarishaji wa mtandao wa mashirika yanayohusika katika msimu wa Hijja.

NCA iliyoanzishwa mwaka wa 2017, ni taasisi ya serikali inayosimamia usalama wa mtandao nchini Saudi Arabia, ambayo imeongeza maandalizi ya Hija.

Saudi Arabia imesema hakutakuwa na kikomo kwa idadi ya mahujaji kutoka kote ulimwenguni kwa msimu ujao wa Hijja, ikirudisha nyuma vizuizi vya mapema vilivyochochewa na janga la ulimwengu.

Takriban Waislamu milioni 2.5 wanatazamiwa kuhudhuria ibada ya Hijja mwaka huu.

3483783

captcha