IQNA

Hija 1444

Mahujaji wanaweza kupokea vyeti vya kukamilisha Hija mtandaoni

15:12 - July 09, 2023
Habari ID: 3477259
MAKKA (IQNA) – Cheti cha kifahari cha Hija kinaweza kutolewa kwa njia ya intaneti kwa wale wote walioshiriki katika Ibada ya Hija mwaka huu wa 1444 Hijria Qamaria.

Wizara ya Hajj na Umrah ya Saudi Arabia imesema Mahujaji wanaotaka kupata cheti wanaweza kufanya hivyo kwa kupakua programu ya Nusuk na kuchagua muundo wa hati wanayopenda.

Wizara iliorodhesha hatua za kupata cheti kupitia programu.

Hajj ya mwaka huu, iliyofanyika mwezi huu wa Dhul Hija iliashiria kurudi kwa idadi ya kawaida Mahujaji katika viwango vyao vya kabla ya janga la Corona.

Saudi Arabia iliondoa ukomo wa idadi na umri wa Mahujaji kutoka kote ulimwenguni kwa Hija ya mwaka huu baada ya COVID-19 au Corona kulazimisha kupunguzwa kwa idadi ya mahujaji kwa miaka mitatu mfululizo.

Takriban Mahujaji milioni 1.8, wakiwemo milioni 1.6 kutoka nje ya Saudia , walihudhuria Hija ya mwaka huu ndani na karibu na mji mtakatifu wa Makka.

Baada ya kukamilisha ibada za Hijja, Mahujaji wengi wa ng’ambo kwa kawaida humiminika kwenye mji mtakatifu wa Madina kusali kwenye Msikiti wa Mtume SAW, eneo la pili takatifu la Uislamu, na kutembelea maeneo mengine Kiislamu katika mji huo.

3484270

Habari zinazohusiana
Kishikizo: hija Hija 1444
captcha