IQNA

Harakati za Qur'ani

Wanaharakati wa Qur'ani wazitaka nchi za Kiislamu kukabiliana na wanaovunjia heshima Qur'ani Tukufu

20:39 - February 08, 2023
Habari ID: 3476532
TEHRAN (IQNA) - Wanaharakati wa Qur'ani Tukufu kutoka Iran na baadhi ya nchi kadhaa katika taarifa yao wamelaani vitendo vya hivi majuzi vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu barani Ulaya, wakizitaka serikali za nchi za Kiislamu kuchukua hatua madhubuti dhidi ya hatua hizo za kufuru.

Taarifa hiyo imetolewa na zaidi ya wataalamu 3,600 wa Qur'ani Tukufu wakiwemo, wasomaji, wahifadhi na walimu kutoka Iran, Syria, Jordan, Misri, Afghanistan, Yemen, Lebanon, Pakistan, Ubelgiji, Kuwait, Bahrain, Saudi Arabia, Iraq, Algeria na Sudan.

Walisema kuzorota ustaarabu wa nchi za Magharibi kwa mara nyingine tena kumedhihirisha safu nyingine ya sura yake ya Kishetani na chafu kutokana na visa hivi vya kuchomwa moto nakala za Qur'ani Tukufu katika nchi kadhaa za Ulaya.

Hatua hizi za fedheha ambazo zilileta lawama na hasira kwa Waislamu duniani kote, hakika hazitabaki bila majibu, ilisisitiza taarifa hiyo.

3482394

Wanaharakati hao wa Qur'ani pia waliwasuta watawala wa nchi za Magharibi wanaoruhusu kuvunjiwa heshima matakatifu ya Kiislamu kwa jina la uhuru wa kujieleza huku wale wanaohoji kuhusu tukio la Holocaust wakifungwa katika nchi za Magharibi.

Walisisitiza uungaji mkono wao kwa Waislamu kote ulimwenguni ambao wameelezea hasira zao na kulaani mpango huu wa Kishetani dhidi ya matukufu ya Kiislamu.

Rasmus Paludan, mwanasiasa mwenye msimamo mkali wa Denmark na Uswidi na kinara wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Stram Kurs (Msimamo Mkali), alichoma nakala ya Qur'ani Tukufu nje ya Ubalozi wa Uturuki mjini Stockholm mnamo Januari 21 kwa ulinzi wa polisi na ruhusa kutoka kwa mamlaka ya Uswidi.

Wiki iliyofuata, alichoma nakala ya kitabu kitakatifu cha Uislamu mbele ya msikiti mmoja nchini Denmark na kusema kuwa atarudia kitendo hicho kila Ijumaa hadi Sweden ijumuishwe katika NATO.

Wakati huo huo, mwanasiasa wa siasa kali za mrengo wa kulia wa Uholanzi Edwin Wagensveld, ambaye ni kinara wa wazungu wenye misimao mikali ya kibaguzi wanaopinga Uislamu katika nchi Magharibi (PEGIDA), aliichana nakala Qur'ani Tukufu kabla ya kuichoma moto katika maandamano ya kupinga Uislamu huko Enschede, Uholanzi mwishoni mwa Januari.

Habari zinazohusiana
captcha