IQNA

Taazia

Amiri wa Kuwait aaga dunia akiwa na miaka 86; kakake ateuliwa kumrithi

22:26 - December 16, 2023
Habari ID: 3478044
IQNA- Amiri wa Kuwait Sheikh Nawaf al-Ahmad al-Jaber al-Sabah amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 86.

Akitangaza habari ya kifo cha kiongozi huyo mkuu wa Kuwait, Waziri wa Mahakkama wa nchi hiyo ya Kiarabu amesema,"Kwa masikitiko na huzuni kubwa, sisi - watu wa Kuwait, mataifa ya Kiarabu na Kiislamu, na watu marafiki wa dunia – tunatangaza kifo cha Sheikh Nawaf Al Ahmad Al Jaber Al Sabah, Amir wa Kuwait ambaye ameaga dunia Jumamosi ya leo,".

Taarifa zaidi zinasema kuwa, kufuatia kifo cha Amir wa Kuwait, serikali ya nchi hiyo imetangaza maombolezo ya kitaifa huku bendera zote zikipeperushwa nusu mlingoti.

Hata hivyo mamlaka za Kuwait hazijatangaza sababu ya kifo cha kiongozi huyo.

Marehemu Sheikh Nawaf aliapishwa Septemba 2020 baada ya kifo cha ndugu yake wa kambo, Sheikh Sabah al-Ahmad al-Jaber al-Sabah aliyefia nchini Marekani akiwa na umri wa miaka 91.

Tayari mwana wa mfalme wa Kuwait na kaka yake wa kambo, Sheikh Meshaal al-Ahmad al-Jaber al-Sabah, 83, ametangazwa kuwa Amir mpya wa Kuwait, imesema taarifa kutoka kwa Issa Al-Kandari, naibu waziri mkuu na waziri wa serikali katika maswala ya baraza la mawaziri.

Kishikizo: kuwait sabah Amir
captcha