IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

Mashindano ya Kuwait ya Qur’ani Yanatarajiwa Kufanyika Novemba

19:41 - October 24, 2023
Habari ID: 3477779
KUWAIT CITY (IQNA) - Toleo la mwaka huu la Tuzo la Kimataifa la Qur'ani Tukufu la Kuwait litafanyika mwezi ujao.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika Jiji la Kuwait siku ya Jumatatu, afisa wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya nchi hiyo ya Kiarabu alisema mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yamepangwa kuandaliwa tarehe 8-15 Novemba.

Muhammad al-Alim alisema itafanyika chini ya uangalizi wa Amir Nawaf Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah wa Kuwait.

Washindani hao watashindana katika kategoria tano zinazojumuisha kuhifadhi Qur'ani Tukufu, usomaji na Tajweed katika viwango tofauti, alibainisha.

Kategoria moja ni mradi bora zaidi unaohudumia Qur’ani Tukufu, kulingana na afisa huyo.

Pia alisema mialiko imetumwa kwa nchi 80 kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo.

Kamati maalum zimeundwa kufanya matayarisho ya kuandaa hafla hiyo ya Qur'ani, Alim alibainisha.

Maonyesho yatafanyika pembezoni mwa mashindano hayo na kutakuwa na hotuba kuhusu masuala ya Qur'ani, aliendelea kusema.

Alim pia alibainisha kuwa programu zilizowekwa pembeni zitajumuisha kuheshimu wanazuoni wa­­ Qur'ani, akiwemo Qari wa Misri Sheikh Ahmed Khalil Shahin Qubais na qari wa kike wa Kuwait Aisha Abdul Rahman al-Safi.

4177388

Kishikizo: kuwait qurani tukufu
captcha