IQNA

Uislamu unavyoenea

Zaidi ya watu 100 Wasilimu nchini Kuwait ndani ya mwaka mmoja

16:46 - December 19, 2022
Habari ID: 3476270
TEHRAN (IQNA) – Maafisa wa Kuwait wanasema jumla ya watu 109 wamesilimu nchini humo tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Kulingana na Jumuiya ya Uhuishaji wa Turathi za Kiislamu ya Kuwait, waongofu hao wapya wanatoka mataifa tofauti.

Wanaume 30 na wanawake 79 waliukubali Uislamu kutokana na mpango ulioitwa "Nifundishe Uislamu", jumuiya hiyo ilisema.

Mpango huo umezinduliwa na Kituo cha Kiislamu cha Al-Hidaya kuwaalika wasio Waislamu kwenye dini hiyo.

Wengi wa wale wanaosilimu kupitia mpango huu wanatoka India na Ufilipino Jumuiya ya Uhuishaji wa Turathi za Kiislamu ya Kuwait ilisema.

Iliongeza kuwa mnamo 2021, wanaume na wanawake 114 walikuwa wamesilimu kupitia mpango wa Al-Hidaya Islamic Center.

Kuwait ni nchi ya Kiarabu yenye Waislamu wengi katika eneo la Ghuba ya Uajemi ambapo Uislamu ndiyo dini rasmi.

4107832

Kishikizo: kuwait waislamu
captcha