
Vikao hivyo vilikuwa sehemu ya Kongamano la Kimataifa Kuhusu Fikra za Qur'ani za Ayatullah Khamenei lililoanza katika mji mtakatifu wa Jumatano na kukamilika leo.
Vikao hivyo vvilivyokuwa na anuani za "Shughuli za Qur'ani katika mawazo ya Ayatullah Khamenei," na "Fikra za Qur'ani za Ayatollah Khamenei katika kazi za wanasemina wa Kiislamu wasio Wairani", vilifanyika katika Ukumbi wa Sheikh Tabarsi wa Wakfu wa Utafiti wa Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Imam Ridha AS maarufu kama Astan Quds Razavi.
Idadi ya wasomi na watafiti wa Iran na wa kigeni waliwasilisha mada zao katika vikao hivyo viwili.
Moja ya makala hizo, iliyoandikwa na Mojtaba Norouzi na Seyed Ali Mousavi Emadi, ilikuwa na uchambuzi wa fahirisi za utekelezaji wa shughuli za Qur'ani kwa mtazamo wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Mousavi Emadi aliyewasilisha mada hiyo amesema kwa kuzingatia kuwa mfumo wa kisiasa, kiutamaduni na kijamii wa jamii nchini Iran umeegemezwa kwenye Qur'ani Tukufu, hatua za kimsingi zaidi zinapaswa kuchukuliwa katika uga wa shughuli za Qur'ani.
Amesema fahirisi za utekelezaji wa shughuli za Qur'ani Tukufu kwa mtazamo wa Ayatullah Khamenei ni pamoja na mtindo wa maisha ya Qur'ani, kuendeleza ustaarabu mpya wa Kiislamu, kukuza ujuzi wa jamii na Kitabu Kitukufu, na kuendeleza tafakari ya Qur'ani.
Hujjatul Islam Roshanzamir, profesa katika Chuo Kikuu cha Sayansi za Kiislamu cha Razavi, aliwasilisha mada kuhusu dhana ya elimu katika Qur'ani na kauli kuhusu "Awamu ya Pili ya Mapinduzi ya Kiislamu".
Mada nyingine ilikuwa ya Mohammad Askari Mumtaz kutoka Pakistan na iliwasilishwa kwa Kiurdu.
Amesema kwa kutumia misingi ya Qur'ani Tukufu ya fikra za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, makala yake inalenga kujibu baadhi ya mashaka na maswali yanayoulizwa na mustashrikeen yaani wasiokuwa Waislamu wanafanya utafiti kuhusu Uislamu na baadhi ya watu wengine nchini India na Pakistan.
Aidha, Abubakr Karambe, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa kutoka Mali, aliwasilisha mada kuhusu suala la usalama katika fikra za Qur'ani za Ayatullah Khamenei.
3486678