IQNA

Ahadi ya Kweli

Meja Jenerali Salami: Uistikbari unatakka kudhibiti utambulisho wa Kiislamu

15:51 - May 09, 2024
Habari ID: 3478795
IQNA-Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) amesema kuwa, ubeberu unaamiliana na ulimwengu wa Kiislamu kwa sera na siasa moja na wala haujali mipaka na kusisitiza kuwa, iwapo adui atadhibiti eneo la Kiislamu basi atapanua hadi sehemu nyingine.

Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda Mkuu wa IRGC amesema hayo mjini Damscus Syria katika shughuli ya Siku ya Arubaini ya mashahidi wa ubalozi mdogo  wa Iran mjini humo na kusisitiza kwamba, uistikbari, ukiongozwa na Marekani,  unataka kudhibiti utambulisho wa Kiislamu.

Meja Jenerali Salami ameongeza kuwa, sisi Waislamu tuko katika meli moja na tuna mahusiano na mafungano sisi kwa sisi na endapo Waislamu wataacha jihadi, basi wataishi kwa udhalili.

Kadhalika Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) ameeleza kuwa, njia na hatima yetu ni moja na hatuwezi kuishi kwa kugawanyika, kwa sababu ikiwa adui atadhibiti eneo la Kiislamu, atapanua udhibiti huo hadi eneo jingine, na kwa hiyo ni lazima tulinde na kuhifadhi vipengele na vielelezo vya nguvu tunayomiliki.

Ikumbukwe kuwa, Jumatatu, Aprili 1, 2024, utawala wa Kizayuni wa Israel ulishambulia sehemu ya ubalozi wa Iran mjini Damascus katika shambulio la kigaidi lililopelekea kuuawa shahidi washauri saba wakuu wa kijeshi wa Iran.
Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran aliitaja hatua ya Israel kuwa ni shambulio dhidi ya ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni "utaadhibiwa".
Katika kutekeleza ahadi hiyo, Jumapili asubuhi (tarehe 14 Aprili 2024), Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu lilichukua hatua ya kuuadhibu utawala huo wa Kizayuni kwa kuvurumisha ndege zisizo na rubani na makombora kuelekea maeneo yanayokaliwa kwa mabavu (Israel) kupitia operesheni ya kuiadhibu Israel iliyopewa jina la Ahadi ya Kweli."

3488246

Habari zinazohusiana
Kishikizo: Ahadi ya Kweli
captcha