Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran siku ya Jumatatu, Esmail Baghaei aliulizwa kuhusu maombi ya nchi mbali mbali ya kuitaka Iran ijuzuie kulipiza kisasi dhidi ya mashambulizi ya anga ya utawala wa Israel.
Baghaei mesema kuna jumbe zinazotumwa kila mara katika uga wa diplomasia, hasa pale kunapokuwa na mvutano, lakini Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kamwe haitajinyima haki yake ya kujibu (uchokozi), ambayo ni haki ya nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa.
Aidha amesema kuwa, sababu kuu ya kiburi na ufidhuli wa utawala wa Kizayuni wa Israel ni uungaji mkono usio na kikomo wa Marekani.
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amebainisha kuwa, viongozi wa Marekani wanapaswa kusimamisha uungaji mmokono na misaada yao ya kisilaha, kijasusi na kisiasa kwa utawala huo ghasibu.
Baqaei ameeleza kuwa, nukta muhimu katika shambuulio la Jumamosi la Israel ni kudhihirika bayana uwezo wa ulinzi wa anga wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Aidha amesema kuhusiana na jinai za Israel kwamba: Mashauriano yote yaliyofanywa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika wiki za hivi karibuni yalilenga kusitishwa mara moja jinai za Israel dhidi ya Gaza na Lebanon, uhamasishaji wa jamii ya kimataifa kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi na kujaribu kuuwajibisha utawala wa Kizayuni kwa sababu tunaamini kwamba, kutochuukuua kwetu hatua za kisheria dhidi ya Israel ndiko kulikoutia kiburi na kuupa kichwa utawala huo ghhasibu.
4244787