Kwa mujibu wa IQNA, Idara ya Uhusiano wa Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika taarifa namba mbili, imetoa maelezo ya kina kuhusu jibu la Iran la makombora dhidi ya Israel kufuatia mauaji ya shahidi Ismail Haniya mjini Tehran na kuuawa shahidi Seyyyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Hizbullah na wenzake katika hujuma ya kigaidi ya Israel huko Beirut, Lebanoni.
Taarifa hiyo ni kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu
Umma wa Kiislamu, Mrengo Adhimu wa Muqawama na Taifa Tukufu la Iran ya Kiislamu
Kufuatia tangazo lililopita, vijana wenu katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kwa mujibu wa ahadi zilizotolewa na maafisa wa Jamhuri ya Kiislamu na makamanda wa kijeshi; Kwa msaada wa vikosi vingine vyenye silaha, wamelenga vituo vya kimkakati ndani ya maeneo yaliyokaliwa kwa makombora yaliyotengenezwa na vijana wa Iran ya Kiislamu wakati wa Operesheni ya Ahadi ya Kweli II kwa kutumia neno la siri la Ya Rasulullah.
Katika operesheni hii, tumelenga baadhi ya vituo vya jeshi la anga na rada; vituo vya kupanga njama na kupanga vitisho dhidi ya viongozi wa muqawama (mapambano ya Kiislamu), haswa shahidi Dakta Ismail Haniya na kiongozi wa Hizbullah ya Lebanon, shahidi Hujjatul Islam wal-Muslimin Seyyed Hassan Nasrallah, na makamanda wa kijeshi wa Hizbullah. , mapambano ya Kiislamu wa Palestina, na makamanda IRGC.
Licha ya kuwa eneo hilo (Israel) linalindwa na mifumo mikubwa na ya hali ya juu zaidi ya ulinzi, asilimia 90 ya makombora yalilenga shabaha kwa mafanikio na utawala wa Kizayuni unatishwa na uwezo wa kiujasusi na kiutendaji wa Jamhuri ya Kiislamu.
Operesheni hii ilifanywa ndani ya mfumo wa haki ya ulinzi halali na kwa kuzingatia sheria za
kimataifa, na adui akifanya ujinga wowote wa kujibu mapigo atakabiliwa na jibu la maangamizi na majuto.”
4240056