Jumanne usiku katika Operesheni Ahadi ya Kweli II makombora ya balestiki ya Iran yalilenga vituo vitatu vya kijeshi karibu na Tel Aviv, mji muu wa utawala ghasibu wa Israel.
"Kwa mujibu wa haki halali na kwa lengo la kuhakikisha amani na usalama kwa Iran na eneo, jibu la uhakika lilitolewa kwa uchokozi wa utawala wa Kizayuni," Pezeshkian aliandika kwenye akaunti yake ya X.
"Operesheni hii ilifanywa kwa ajili ya kutetea maslahi ya Iran na raia. Hebu (Waziri Mkuu wa Israel) Netanyahu afahamu kwamba Iran haitaki vita, lakini inasimama kidete dhidi ya tishio lolote. Hii ni sehemu tu ya nguvu zetu. Usijihusishe na mzozo na Iran."
Makombora ya Iran yamelenga Israel kujibu mauaji ya viongozi waandamizi wa muqawama au harakati za mapambano ya Kiislamu ambayeo yametekellezwa na utawala ghasibu wa Israell, na ukatili wake katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa na mashambulizi ya kiakili ya Lebanon.
Jeshi la Iran Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetoa taarifa muda mfupi baada ya kuanza kwa mashambulio ya makombora ya kulipiza kisasi Jumanne jioni.
Taarifa ya IRGC imsema mashambulizi hayo dhidi ya Israel yalikuwa ni kujibu kuuawa shahidi kwa mkuu wa Hamas aliyeuawa kigaidi Tehran, Ismail Haniyah, kiongozi wa Hizbullah Sayyid Hassan Nasrallah, na kamanda mwandamizi wa IRGC Abbas Nilforoushan ambaye aliuawa shahidi akiwa na Nasrallah jijini Beirut Ijumaa katika hujuma ya kigaidi ya Israel.
Jeshi la Wanaanga la IRGC limerusha makumi ya makombora ya balestiki yakilenga vituo muhimu vya kijeshi na kijasusi vya Israel katikati mwa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu.