IQNA

Operesheni ya Ahadi ya Kweli II

Araghchi: Makombora ya Iran ni jibu kwa ugaidi wa Israel

12:25 - October 02, 2024
Habari ID: 3479524
IQNA-Waziri wa Iran wa Mashauri ya Kigeni  amesema pambizoni mwa kikao cha leo cha Baraza la Mawaziri kuhusiana na Operesheni Ahadi ya Kweli II kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetumia tu haki yake ya kujihami kihalali kujibu harakati za kigaidi za utawala wa Kizayuni wa Israel ndani ya Iran.

Seyyed Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje, ameashiria  madai ya baadhi ya nchi za eneo kama vile Jordan, kuhusu kutungua makombora ya Iran yaliyokuwa yakielekea katika ngome za Israel na kusema: ‘Ukweli ni kwamba walishindwa kuzuia zaidi ya asilimia 90 ya makombora na hivo makombora yaligonga shabaha.”

Amendelea kusema kuwa, Iran imeziambia nchi nyingine kwamba yeyote anayeruhusu nchi yake itumiwe na maadui dhidi ya Iran atahesabiwa kuwa ni adui.

Wakati huo huo,  Araghchi amelitaja shambulio kali la makombora la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya utawala katili wa Israel kuwa limeendana na haki ya halali wa kujilinda ya Kifungu cha 51 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa (UN).

Araghchi amesema hayo katika mazungumzo aliyofanya kwa njia ya simu na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Ujerumani na Ufaransa akiashiria namna Iran ilivyoonyesha stahamala kwa zaidi ya miezi miwili kufuatia jinai za mara kwa mara zilizofanywa na utawala wa Kizayuni mjini Tehran na katika Ukanda wa Gaza na Lebanon, na akasema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelenga vituo vya kijeshi na usalama vya utawala wa Kizayuni.

Mkuu wa chombo cha kidiplomasia cha Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitaki kushadidisha mivutano na vita hata kama haina hofu ya vita na akasisitiza kwamba iwapo utawala wa Kizayuni utajaribu kuchukua hatua ya kulipiza kisasi, jibu la Iran litakuwa kali zaidi.

Kwa mara nyingine tena, Araghchi ametoa wito kwa nchi zote kufanya juhudi za kusimamisha vita, kuzuia mashambulizi ya utawala wa Kizayuni na kuepusha kushadidi zaidi mivutano katika eneo hususan Lebanon na huko  Ukanda wa Gaza.

Kuhusiana na suala hilo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Araghchi ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba Tehran imechukua hatua hiyo baada ya takriban miezi miwili ya kujizuia kulipiza kisasi na ili kutoa fursa ya uwezekano wa kusitishwa mapigano huko Ukanda wa  Gaza.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) jana Jumanne usiku Oktoba Mosi lilitoa taarifa na kutangaza kuwa: katika kutoa jibu kwa hatua ya kuwaua shahidi Mujahid Ismail Hania, Sayyid Hassan Nasrullah na Abbas Nilfourusha Mkuu wa operesheni za IRGC imezilenga ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel).

Kwa mujibu wa tangazo la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, asilimia 90 ya makombora hayo yalifanikiwa kulenga shabaha zilizokusudiwa katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu.

4240188

Habari zinazohusiana
captcha