IQNA

Ahadi ya Kweli

Operesheni ya Iran ya Ahadi ya Kweli imesembaratisha dhana potofu ya kutoshindwa Israel

10:52 - April 18, 2024
Habari ID: 3478697
IQNA – Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Lebanon amepongeza shambulio la hivi karibuni la Iran dhidi ya Israel kwa kutumia makombora na ndege zisizo na akisema kwamba limesambaratisha dhana potofu ya kutoshindwa kijeshi utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika taarifa yake, Jahad Zabyan alibainisha kuwa shambulio hilo ambalo halijawahi kushuhudiwa, lililopewa jina la "Operesheni Ahadi ya Kweli", lilifanywa na jeshi la Iran kujibu mashambulio ya utawala wa Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran huko Damascus, Syria. Amesema operesheni hiyo imepata mafanikio mengi hasa  kuthibitisha kuwa utawala wa Israel hauna uwezo wa kujilinda wenyewe, alisema.

Kwa kutekeleza "Operesheni ya Ahadi ya Kweli ", Iran ilituma ujumbe kuhusu mwanzo wa enzi mpya katika makabiliano yake na Israel, alisema.Mwanasiasa huyo wa Lebanon aidha amebainisha kuwa Iran ilitumia sehemu ndogo tu ya uwezo wake wa kijeshi katika operesheni hiyo na Waisraeli na washirika wao hususan Wamarekani walilitambua hilo vyema.

Vile vile ameashiria athari za mashambulizi ya Iran kwa Israel katika kupunguza wigo wa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza, akisema huo unaweza kuwa mwanzo wa kumalizika vita vya Gaza.

Kwingineko katika matamshi yake, Zabyan alizikosoa baadhi ya nchi za Kiarabu zilizoshiriki kuihami Israel dhidi ya makombora na ndege zisizo na rubani za Iran, akisema anatamani badala yake zingetumia uwezo wao kuzuia kuendelea kwa vita vya mauaji ya halaiki ya Israel dhidi ya Gaza ambavyo vimesababisha vifo vya takriban Wapalestina 40,000 wengi wakiwa ni wanawake na watoto huku wengine takribani laki moja wakijeruhiwa.

Aprili Mosi utawala wa Kizayuni ulifanya shambulizi la kigaidi dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran huko Damascus, mji mkuu wa Syria, na kupelekea kuuawa shahidi washauri saba wa kijeshi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC)  ambao walikuwa nchini Syria kwa mwaliko wa serikali ya nchi hiyo. Katika kujibu jinai hiyo mapema Jumapili tarehe 14 April 2024 Iran ilifanya mashambulizi ya moja kwa moja ya ndege zisizo na rubani na makombora dhidi ya Israel.

Operesheni hiyo ya kijeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliyopewa jina la Ahadi ya Kweli ilikuwa haki yake ya kimsingi ya kujilinda, ambayo imeelezwa wazi chini ya Ibara ya 51 ya Hati ya Umoja wa Mataifa na katika kukabiliana na uchokozi wa kijeshi wa mara kwa mara wa utawala wa Israel, hasa mashambulizi ya kijeshi ya utawala huo dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran, mashambulizi ambayo ni kinyume kabisa cha kifungu cha 2 ibara ya 4 ya hati hiyo.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Meja Jenerali Hossein Salami ameuonya utawala wa Israel kwamba jibu la Iran litakuwa "kali zaidi" ikiwa utawala huo utatoa jibu kwa operesheni ya kulipiza kisasi ya Iran. Salami alisisitiza kwamba Iran inaweza kufanya operesheni kwa kiwango kikubwa zaidi lakini shambulio hilo "lilikuwa na mipaka" kwa kambi za kijeshi za utawala wa Kizayuni, kutoka Miinuko ya Golan hadi Jangwa la Negev, ambazo zilitumiwa katika shambulio la kigaidi kwenye ubalozi mdogo wa Iran jijini Damascus.

Duru zinadokeza kuwa, makombora yote ya hypersonic yaliyotumiwa katika mashambulizi ya Iran ya kuiadhibu Israel yalipiga shabaha zilizokusudiwa baada ya kukwepa mifumo ya ulinzi ya anga ya utawala huo haramu na washirika wake. Mkuu wa Majeshi ya Iran, Meja Jenerali Mohammad Baqeri, alithibitisha kwamba Iran imepiga kambi kubwa ya kijasusi ya Israel na kituo cha anga cha Nevatim, ambako ndege ya F-35 ilitokea na kulenga majengo ya kidiplomasia ya Iran huko Damascus.

 

4210522   

   

Kishikizo: Ahadi ya Kweli
captcha