IQNA

Operesheni ya Ahadi ya Kweli II

Iran yashusha mvua ya makmbora kote 'Israel'

21:53 - October 01, 2024
Habari ID: 3479519
TEHRAN- Ving'ora vinasikika katika kote Israel (ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu) baada ya majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuvurumisha idadi kubwa ya makombora ambayo yamelenga ngome muhimu za kijeshi za utawala wa Kizayuni wa Israel

Anga ya Tel Aviv imegubikwa na makombora na milipuko ilisikika katika eneo la al-Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu na kuwafanya walowezi wa Kizayuni katika miji hiyo miwili na kote Israel kukimbilia katika maficho ya chini ya ardhi.

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ya Israel imesema hakuna ndege itakayoruhusiwa kupaa au kufika katika viwanja vyote vya ndege vya Israel.

Gazeti la Kizayuni la Haaretz liliripoti "vipigo vya moja kwa moja" huko Negev, Sharon na maeneo mengine kufuatia shambulio la makombora kutoka Iran.

Mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel maarufu kama Kuba la Chuma (Iron Dome) umeshindwa kutungua makombora ya Iran.

Jeshi la Iran Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetoa taarifa muda mfupi baada ya kuanza kwa mashambulio ya makombora ya kulipiza kisasi Jumanne jioni.

Taarifa ya IRGC imsema mashambulizi hayo dhidi ya Israel yalikuwa ni kujibu kuuawa shahidi kwa mkuu wa Hamas aliyeuawa kigaidi Tehran, Ismail Haniyah, kiongozi wa Hizbullah Sayyid  Hassan Nasrallah, na kamanda mwandamizi wa IRGC Abbas Nilforoushan ambaye aliuawa shahidi akiwa na Nasrallah jijini Beirut Ijumaa katika hujuma ya kigaidi ya Israel.

Jeshi la Wanaanga la IRGC limerusha makumi ya makombora ya balestiki yakilenga vituo muhimu vya kijeshi na kijasusi vya Israel katikati mwa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu.

IRGC imesema operesheni hiyo ya leo ya makombora ilienda sambamba na haki ya Iran ya kujilinda kihalali kulingana na Mkataba wa Umoja wa Mataifa, na kujibu uhalifu unaoongezeka wa utawala ghasibu wa Israel - unaoungwa mkono na Marekani - dhidi ya watu wa Lebanon na Wapalestina wa Gaza.

IRGC imesema utawala wa Kizayuni wa Israel utakabiliwa na mashambulizi makali zaidi endapo utachukua hatua ya kijeshi dhidi ya Iran.

Ofisi ya Mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa imesema katika taarifa yake kwamba operesheni hiyo ya makombora iilikuwa jibu la "kisheria, kimantiki na halali" kwa vitendo vya kigaidi vya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Pia iliuonya utawala wa Israel kwamba jibu la "kuponda" zaidi litatekelezwa iwapo utathubutu kujibu au kufanya vitendo zaidi vya udhalimu.

 4240047

Habari zinazohusiana
captcha