IQNA

Mbunge apongeza Jeshi la Ulinzi wa Anga Iran kwa kuzima uchokozi wa Israel

15:22 - October 26, 2024
Habari ID: 3479647
IQNA – Mbunge wa ngazi za juu katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (bunge la Iran) amepongeza kikosi cha ulinzi wa anga cha Iran kwa kufanikiwa kuzima shambulio la anga la utawala haramu Israel Jumamosi asubuhi.


Akilaani kitendo cha uchokozi cha utawala wa Kizayuni, Alaeddin Boroujerdi, mjumbe wa tume ya usalama wa taifa na sera za kigeni katika bunge hilo, amezungumza na IQNA na kusema kwamba Iran inahifadhi haki ya kukabiliana na uchokozi huo kwa kuzingatia sheria za kimataifa.
Vile vile amesema kuwa majibu ya vikosi vya ulinzi vya anga vya Iran kwa mashambulizi hayo yanathibitisha uwezo wa kiulinzi wa nchi hiyo.
Vikosi vya ulinzi wa anga nchini vimekabiliana na uchokozi wa utawala wa Israel na kuzuia makombora yaliyorushwa, alisema.
Jibu hilo la Iran ambalo limtolewa kwa wakati limeonyesha uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu ya kuendeleza hatua za ulinzi katika kukabiliana na hujuma za maadui, aliongeza.
Boroujerdi ameema wakati utawala wa Kizayuni unaoungwa mkono na Marekani umekuwa ukijigamba juu ya uwezo wake wa kijeshi, lakini vikosi vya kijeshi vya Iran vilisambaratisha sura ghushi ya utawala huo kwa kutekeleza Operesheni za Ahadi ya Kweli.
Idara ya Mahusiano ya Umma ya Ulinzi wa Anga wa Iran imetoa taarifa ikisema kuwa leo Jumamosi alfajiri utawala wa Kizayuni wa Israel umeshambulia vituo vya kijeshi vya mikoa ya Tehran, Khuzestan na Ilam ikiwa ni katika kuzidisha hali ya mvutano katika eneo, ambapo mfumo wa ulinzi wa anga wa Jamhuri ya Kiislamu ya  Iran umeweza kukabiliana kwa mafanikio na kitendo hicho cha kichokozi cha utawala wa Kizayuni.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mashambulizi hayo yamesababisha uharibifu mdogo katika baadhi ya maeneo na uchunguzi unaendelea kufanywa kubaini uzito wa tukio hilo.
 4244355

Habari zinazohusiana
captcha