Rais Ebrahim Raisi amesema hayo alipokutana na hadhara ya waandishi na shakhsia mashuhuri wa kifasihi na kiutamaduni katika Ulimwengu wa Kiislamu ambao waliokuja Iran kushiriki katika Maonesho ya 35 ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran na kubainisha kuwa, adui leo anafanya njama za kuongoza maoni ya umma ya mataifa juu ya suala la Gaza, kwa himaya ya vyombo vya habari, habari za uongo, simulizi zisizo za kweli, na upotoshaji wa ukweli.
Rais Ebrahim Raisi amesisitiza umuhimu wa nafasi na wajibu wa waandishi na wana utamaduni katika kukabiliana na njama hii chafu.
Aidha amesema, kusimama kidete watu wa Palestina, muqawama wao, imani yao kwa Mwenyezi Mungu naa juhudi za kambi ya muqawama zinahitaji simulizi sahihi na za kisanii, na kuongeza kuwa simulizi hii inahitaji juhudi za washairi, waandishi na watu wa kitamaduni katika ulimwengu wa Kiislamu.
Rais wa Iran ameashiria matukio ya sasa ya Gaza na kueleza kwamba, Palestina leo ni suala la kwanza na la pamoja kwa nchi zote za Kiislamu.
Kadhalika Ebrahim Raisi amesema, kudumishwa umoja na mshikamano huu katika ulimwengu wa Kiislamu ni chimbuko la ushindi wa taifa la Palestina
3488353