IQNA

Hija ya Mwaka 1445

Mipango ya Hija ya Mwaka Ujao Kuanza Hivi Karibuni

10:42 - June 20, 2024
Habari ID: 3478991
IQNA-Upangaji wa Hija ya mwaka ujao utaanza mara tu baada ya mafanikio ya hija mwaka huu kumalizika, afisa mmoja wa Saudia amesema.

Naibu Amir wa Makka  na Naibu Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Hija ya Saudi Saud bin Mishal alitangaza siku ya Jumanne mafanikio ya Hija ya mwaka huu.

Amesema: “Ninafuraha kutangaza mafanikio ya msimu wa Hija wa mwaka huu na natoa sifa zangu kwa Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kutekeleza jukumu letu la juu kabisa kwa wageni wa Mwenyezi Mungu na kutuheshimu kwa kuwahudumia na kuwezesha utekelezaji wa ibada ya faradhi katika mazingira salama na yenye amani.

Hali kadhalika Naibu Amir wa Makka alisema kuwa; mipango ya msimu wa Hija wa mwaka ujao itaanza mara moja mara baada ya kumaliza hii.

Kwa hivyo mafanikio yaliyopatikana katika ngazi zote ni mwanzo tu wa awamu mpya ya kufikia mafanikio makubwa, katika kuwahudumia mahujaji na mwenyzi mungu akipenda, kazi itaanza mara moja kupanga kwa ajili ya msimu wa Hija wa mwaka ujao na tutaendelea kuendeleza mfumo mzima wa Hija, aliongeza kwa kusema;

Hija ni safari ya kwenda Makka ambayo kila Mwislamu mwenye uwezo wa kimwili na uwezo wa kifedha analazimika kuitekeleza angalau mara moja katika maisha yake.

3488808

Kishikizo: hija makka umrah 1445
captcha