IQNA

Milango 199 yazinduliwa Misikiti ya Makka na Madina ili kuboresha mtiririko wa Mahujaji

21:55 - May 31, 2025
Habari ID: 3480768
IQNA – Jumla ya milango 199 imewezeshwa ili kuboresha mtiririko wa Mahujaji wanaoingia na kutoka katika Msikiti Mkuu wa Makka, Masjid al Haram na Msikiti wa Mtume, Al Masjid an Nabawi, huko Madina wakati wa msimu wa Hija.

Wakati mamilioni ya Mahujaji wanajiandaa kumiminika katika maeneo matakatifu kwa ajili ya ibada ya Hija mwaka huu, Mamlaka Kuu ya Saudi Arabia inayosimamia misikiti hiyo miwili mitakatifu imetangaza mpango mpana wa uwanja unaolenga kuhakikisha hali salama na ibada yenye utulivu kwa waumini wote. 

Mamlaka hiyo ilielezea huduma na maboresho kadhaa yaliyoletwa katika Msikiti Mkuu wa Makka na Msikiti wa Mtume huko Madina, ili kuhakikisha viwango vya juu vya mpangiliIo na urahisi wa kuingia nakutoka Mahujaji.. 

Maandalizi hayo yanajumuisha maeneo 13 maalum ya kuswali yaliyotengwa kwa ajili ya watu wenye ulemavu, ili kuhakikisha kila muumini anaweza kushiriki ibada kwa usawa. Ili kurahisisha harakati ndani ya misikiti hiyo, mamlaka hiyo imeweka lifti 22 na ngazi za umeme 224. Kutambua utofauti wa lugha katika umma wa Kiislamu duniani, nyaraka za kidini na kielimu zitapatikana katika lugha 27, kusaidia Mahujaji wa kimataifa kushiriki kikamilifu katika ibada hii muhimu. 

Kwa jumla, milango 199 imefunguliwa ili kuboresha mtiririko wa Mahujaji wanaoingia na kutoka kwenye misikiti, kuwezesha udhibiti bora wa umati wakati wa nyakati za kilele. 

Ili kuhakikisha faraja katikati ya joto la jangwani, zaidi ya vitengo vya kupoza hewa 883, mashine za kupuliza ukungu 244, na mashinie 3,139 za uingizaji zimewekwa katika maeneo matakatifu. Aidha, vifaa 432 vya kupuliza manukato vitatumika ili kuboresha mazingira ya utulivu na ibada. 

Aidha magari ya umeme 400 yatatoa msaada wa ziada kwa Mahujaji wazee na wale walio na ulemavu wa mwili ili kukamilisha ibada zao. 

Kwa upande wa usalama, mamlaka hiyo imeweka kimkakati vifaa 1,229 vya dharura katika maeneo yenye msongamano mkubwa na imeunganisha mtandao wa sauti wa ubora wa juu wenye spika 8,000 ili kutoa maelekezo wazi na ujumbe wa kidini katika kipindi chote cha Hajj. 

Maktaba za misikiti zinaendelea kuwa kiini cha utafiti wa Kiislamu na uhifadhi wa utamaduni, zikipatia waumini fursa ya kufikia hati adimu 8,503 kama sehemu ya mpango wa kidijitali unaoendelea. Ili kuongeza mwangaza na usalama, zaidi ya taa 120,000 zitawashwa kwa mujibu wa mahitajio katika maeneo hayo matakatifu na majengo yanayozunguka.  

3493282

Kishikizo: makka madina hija
captcha