Muislamu hachukui hatua hizi kwa kulazimishwa na wengine, bali kwa sababu ya uwepo wake katika jamii na amri aliyoitoa Mwenyezi Mungu.
Wajibu wa kijamii ni aina ya wajibu wa kimaadili na wa kijamii ambapo watu wanawajibika kwa wanadamu wenzao.
Kwa kuzingatia wajibu huu, mtu anapaswa kufanya mfululizo wa vitendo kwa maslahi ya jamii.
Katika maisha ya kijamii, hatima ya kiuchumi, kitamaduni na kiitikadi ya watu imeunganishwa, na vitendo na tabia ya kila mtu huathiri wanajamii wengine katika maeneo tofauti.
Kwa hiyo, watu katika jamii wanawajibika kwa tabia na matendo ya kila mmoja wao.
Kwa kuzingatia mafundisho ya Uislamu, wajibu wa kijamii unajumuisha mfululizo wa tabia na matendo ambayo watu huwafanyia wanadamu wenzao.
Vitendo hivi vina msingi wa aya za Qur’ani, kuanzia hisia ya uwajibikaji kwa familia na jamaa hadi hisia ya uwajibikaji kwa wanajamii wote.
Katika fikira za Kiislamu, Muislamu hapaswi kupuuza matatizo au upungufu katika masuala ya kijamii na mahusiano ya kibinadamu, bali ajaribu kuyashughulikia.
Mfano mmoja wa uwajibikaji kama huo wa kijamii, kwa mujibu wa Qur’ani, ni kuwa na shauku ya kujitolea kwa mayatima na maskini. Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 34 ya Surah Al-Isra: “Wala msiyakaribie mali ya yatima, isipo kuwa kwa njia iliyo bora, mpaka afike utuuzimani. Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itasailiwa."
Wajibu wa kijamii kuhusu mayatima ni muhimu sana kiasi kwamba baadhi ya wafasiri wa Qur’ani wanasema kwamba Sura Al-Maoun inajenga mafungamano yenye nguvu kati ya imani kwa Mwenyezi Mungu, kuwahudumia mayatima, masikini na wafungwa wa vita, na kukubalika kwa Swalah.
Hii inaashiria kwamba imani ya kweli ya kidini inategemea kuzingatia masuala ya jamii na kujaribu kuwasaidia wanadamu wenzako kutimiza mahitaji yao muhimu. Iwapo mtu atapuuza na kutojali kuhusu wanadamu wenzake katika jamii, imani yake, Swalah na matendo ya ibada si ya kweli kwa sababu yanakosa kipengele muhimu cha huruma na kuwasaidia wengine.
Mfano mwingine wa uwajibikaji wa kijamii katika Qur’ani ni suala la Tawasi, ambalo maana yake ni kutoa ushauri. Qur’ani katika aya nyingi inawataka Waislamu kufanya Tawasi na kulingania wao kwa wao kwenye masuala kama vile subira na (kusimamia) ukweli.
Tawasi husaidia kuimarisha azimio na hamasa ya wengine pale wanapokabiliwa na matatizo na dhamira yao ni dhaifu.
Kwa ujumla, suala la uwajibikaji wa kijamii limepewa mazingatio maalum katika Uislamu, na msisitizo huu wa kuwajali wengine na kwa jamii unaweza kuwa ni sababu mojawapo ya kuendelea na kubakia kwa dini.
3489660