IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Rais wa Tanzania ahutubu katika Mashindano Ya Kimataifa Ya Qur’ani kwa wasichana

22:52 - September 01, 2024
Habari ID: 3479364
IQNA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan, jana Agosti 31, 2024 alishiriki katika hafla ya kufunga Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu kwa wanawake na washichana yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu ya Rais, katika hotuba yake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt. Samia amesema kuwa Taasisi za kidini zina wajibu mkubwa katika kulinda misingi ya familia na kujenga Taifa lenye maadili. 

Katika hafla hiyo kumetolewa  tuzo kwa washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya kusoma Quran Tukufu kwa wasichana, yaliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa kushirikiana Taasisi ya World Muslim League ya Saudi Arabia.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Aidha, Rais Dkt. Samia ametoa wito kwa BAKWATA kuweka mikakati ya kufundisha elimu ya dini kwa watoto wote bila ubaguzi na kusisitiza umuhimu wa elimu ya dini kwa wanawake kwa kuwa wanawake wana nafasi kubwa katika ulezi wa familia bora.

Vile vile, Rais Dkt. Samia ameeleza kuwa, kumlea mtoto wa kike katika misingi mizuri ya kiimani kunamuandaa kuishi katika misingi hiyo. Hivyo, ni muhimu kuendelea kuimarisha familia ambayo ni msingi wa Taifa letu, ikiwemo kupitia elimu ya dini.

Akizungumzia mashindano hayo yaliyofanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, Rais Dkt. Samia amebainisha kuwa, kuchanguliwa kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa kwanza wa mashindano hayo ni kutokana sifa kubwa ya Tanzania ya kuishi kwa amani na masikilizano.

Rais Dkt. Samia amewataka Watanzania waendelee kulinda heshima hiyo kwa kudumisha amani na mshikamano.

Nafasi ya kwanza katika mashindano hayo imechukuliwa na Bi. Amina Yekhlef wa Algeria.

Rais Samia ahudhuria Mashindano ya Dunia ya Qur’an tukufu kwa Wanawake. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwakabidhi zawadi washindi wa mashindano ya Dunia ya Qur’an tukufu kwa wasichana yaliyofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Agosti, 2024.

 

4234598

Habari zinazohusiana
captcha