IQNA

10:38 - May 24, 2018
News ID: 3471529
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tanzania yanatazamiwa kufanyika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mjini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa, mashindano hayo ambayo yanajulikana kama 'Zawadi ya  Kimataifa ya Tanzania ya Qur'ani Tukufu' yatafanyika kwa muda wa wiki moja kuanzia Mei 31 sawa na Ramadhani 16-22 mwaka 1439 Hijria.

Nchi kadhaa, hasa nchi jirani zinatazamiwa kushiriki katika mashindano hayo ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu. Mwaka jana mashindano hayo yalikuwa na washiriki kutoka nchi zaidi ya 20.

Watanzania wamekuwa wakifanikiwa katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani katika miaka ya hivi karibuni na hivyo kufanyika mashindano hayo kumetathminiwa kama hatua muhimu ya kuimarisha maarifa ya Qur'ani katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

3716622

Name:
Email:
* Comment: