Taasisi ya Aisha Sururu iliandaa hafla hiyo, ambayo sherehe zake za kufunga zilihudhuriwa na wabunge kadhaa.
Washindani walishindana katika kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika ngazi 8 (kuhifadhi Juzuu 1, Juzuu tatu, Juzuu tano, Juzuu saba, Juzuu kumi, Juzuu 15, Juzuu 20, Juzuu 25 na Juzuu zote 30 za Qur'ani Tukufu
Washindi wa safu tatu za juu katika kila ngazi walitunukiwa katika hafla hiyo iliyofana.
Haya yalikuwa mashindano ya pili ya Qur'ani kwa wanawake jijini Dar es-Salaam ndani ya miezi miwili.
Ya awali ilifanyika Julai na yaliandaliwa na Taasisi ya Umm al-Mumineen na kuhudhuriwa na maafisa kadhaa wa serikali pamoja na viongozi mbali mbali wa kidini.
Jiji hilo pia litaandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kwa wanawake wa nchi za Afrika mwezi Septemba.
Kutakuwa na washiriki kutoka nchi 11 za Afrika watakaoshindana katika mashindano yajayo ya kimataifa.
Katika miaka ya hivi karibuni Tanzania imekuwa mwenyeji wa mashindano kadhaa ya kitaifa na kimataifa ya Qur'ani Tukufu.