IQNA

Mashindano ya Qurani yafanyika Zanzibar, Tanzania

0:09 - December 03, 2016
Habari ID: 3470712
IQNA-Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani yamefanyika mapema wiki hii visiwani Zanzibar nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, washiriki 98 walishiriki katika mashindano ya kuhifadhi Qur'ani ambapo kulikuwa na vitengo tafauti vya wanawake na wanaume.
Taarifa zinasema ashindano hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani ikishirikiana na Jumuiya ya Kuhifadhi na Kusomesha Qur'ani Zanzibar.
Washiriki walishindana katika kuhifadhi Qur'ani Kikamilifu na pia kuhifadhi Juzuu 25, 20, 15, 10, 5 na 3 za Qur'ani Tukufu.
Aidha Maustadhi wa hadhi ya juu walisimamia zoezi hilo kama majaji na baada ya hapo washiriki wakapokea zawadi katika sherehe za kufunga mashindano hayo ambazo pia zilihudhuriwa na maafisa wa serikali na wanazuoni wa Kiislamu.
 

captcha