Mashindano haya yaliandaliwa na Idara ya Masuala ya Kielimu na Kitamaduni ya Haram Takatifu ya Hadhrat Abbas (AS).
Sayyid Dhurgham Al-Ibrahimi, mkuu wa Mradi wa Qur'ani katika Kituo cha Masomo ya Kiafrika kinachohusiana na idara hiyo, alisisitiza malengo ya tukio hilo. "Mashindano haya yanaendana na juhudi za kituo cha kuendeleza maarifa ya Qur'ani kote katika bara la Afrika na kuimarisha ushirikiano wa kijamii na Qur'ani Tukufu," alisema.
Al-Ibrahimi alieleza kuwa kituo hicho kinalenga kukuza uelewa wa Qur'ani miongoni mwa vijana na watoto wa Afrika. "Tumejizatiti kuandaa kozi na mashindano ya Qur'ani kote Afrika ili kupanua wigo wa mafundisho ya Qur'ani," aliongeza.
Katika hafla ya kufunga iwashiriki watatu bora walitunukiwa zawadi huku wote waliohudhuria wakienziwa.
Akizungumza katika hafla hiyo, Sheikh Kiza Musa Kiza, mratibu wa kituo hicho nchini Tanzania, alisifu juhudi za washiriki. Alibainisha umuhimu wa mipango kama hiyo katika kukuza utamaduni wa Qur'ani miongoni mwa vizazi vya vijana.
3491443