IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya 21 ya Kimataifa ya Usomaji wa Qur'ani Tukufu kufanyika Tanzania

11:43 - January 03, 2025
Habari ID: 3479996
Mashindano ya 21 ya Kimataifa ya Usomaji wa Qur'ani Tukufu yatafanyika Machi mwaka huu katika jiji la Dar es Salaam, Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa za IQNA, mashindano haya maarufu yanaandaliwa na Taasisi ya Khidmat Al-Quran ya Tanzania. Mashindano haya yanatarajiwa kuanza tarehe 15 Machi 2024 katika jiji la Dar es Salaam. Kama ilivyotangazwa kwenye ukurasa wa Instagram wa taasisi hiyo, washiriki kutoka Lebanon, Afrika Kusini, Pakistan, Malaysia, Yemen, Mali, Misri, Iraq, Afghanistan, Uturuki, na Morocco watahudhuria.

Mwaka huu, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi na Sheikh Yasser Al-Sharqawi, msomaji maarufu wa Quran kutoka Misri, watakuwa wageni rasmi wa mashindano hayo.

Mashindano haya yanachukuliwa kuwa tukio maarufu zaidi la usomaji wa Qur'ani nchini Tanzania na Afrika Mashariki, yakiratibiwa na Taasisi ya Khidmat Al-Quran, taasisi isiyo ya kiserikali ya Kiislamu inayojitolea kukuza elimu na utamaduni wa Qur'ani nchini Tanzania.

 

Katika miaka ya hivi karibuni, taasisi hiyo imeandaa matukio mbalimbali ya Qur'ani, ikiwa ni pamoja na mashindano ya kitaifa na kimataifa ya usomaji na uimbaji wa Qur'ani. Taasisi hiyo pia imechangia kwa kiasi kikubwa kuinua hadhi ya Tanzania katika jamii ya kimataifa ya Qur'ani kwa kuwaalika wasomaji mashuhuri wa Quran nchini.

Kwa mfano, mwaka jana, Sheikh Mahmoud Shahat Anwar alialikwa kama mgeni wa Taasisi ya Khidmat Al-Qur'ani, ambapo usomaji wake ulipokelewa kwa pongezi kubwa miongoni mwa Waislamu wa Tanzania.

4257720

Habari zinazohusiana
captcha