Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo katika ujumbe wake wa shukurani kwa ukarimu wa taifa na serikali ya Iraq katika Arbaeen ya Imam Hussein (AS).
Ayatullah Khamenei amesema: "Neno la kwanza ni asante; ninakushukuru kutoka ndani ya moyo wangu, kwa niaba yangu na kwa niaba ya taifa kubwa la Iran: Nyinyi, waandaaji wa mawkib (vipanda vya utoaji huduma kwa wafanyaziara), ambao mmeleta utu, rehema na wema kwa kiwango cha juu kabisa katika masiku ya kumbukumbu ya Arbaeen ya Imam Hussein (AS)."
Kiongozi Muadhamu ameendelea kusema kuwa: "Kama ambavyo ninatoa shukurani zangu kwa taifa lote kubwa la Iraq na kuanzia maafisa katika serikali ya Iraq ambao wametoa usalama, nafasi na kuandaa mazingira; hususan kutoka kwa wanavyuoni watukufu na mamlaka kubwa za Iraq ambazo zimeandaa mazingira ya kufanya ziara na kuweko anga ya udugu baina ya watu na baina ya mataifa mawili; kwa hakika ni jambo la kushukuru."
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: "Mienendo yenu ndugu wapendwa wa Iraq katika mawkib, njia na tabia yenu ya ukarimu kwa mazuwwar (wafanyaziara) wa Imam Hussein (AS), haina kifani katika ulimwengu wa leo, kama ambavyo matembezi yenyewe ya Arbaeen ya Imam Hussein (AS) hayana kifani katika historia, na kama ambavyo kulinda usalama na afya ya makumi ya mamilioni ya watu katika ulimwengu wa sasa usio na usalama, ni jambo kubwa na la kipekee."
Arbaeen ni tukio la kidini ambalo aghalabu huadhimishwa na Waislamu wa madhehebu Shia katika siku ya arubaini baada ya Siku ya Ashura, kumbukizi ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) na imamu wa tatu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia.
Ni miongoni mwa mjumuiko mkubwa zaidi za kila mwaka duniani, huku mamilioni ya Waislamu wa madhehebu ya Shia, pamoja na Masunni wengi na wafuasi wa dini nyinginezo wakitembea kuelekea Karbala kutoka miji mbalimbali ya Iraq na nchi jirani. Mwaka huu, siku ya Arbaeen iliangukia tarehe 25 Agosti.
Maafisa wa Iraq wanasema mwaka huu takribani wafanyaziara milioni 21 walishiriki katika ziyara na matembezi ya Arbaeen.
3489868