Kwa takriban wiki mbili, Waislamu kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Iran, Afghanistan, Azerbaijan, Bahrain, Kuwait, Pakistan, nchi za Afrika kama Tanzania na Kenya, India, nchi za Ulaya na Saudi Arabia, wamekuwa wakiwasili katika mji huo, ulioko kilomita 100 kusini magharibi mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad, kwa ajili ya kumbukumbu ya Siku ya Arubaini ya Imam Hussein inayosadifiana na leo tarehe 25 Agosti
Waislamu hao husafiri hadi katika mji huo mtakatifu ili kupata nafasi ya kugusa ziara na uzio wa rangi ya dhahabu unaozunguka kaburi la Imam Hussein. Waislamu hao wanaonekana wakiwa wamebeba vifurushi vyao kwenye mikoba au mifuko kuelekea Karbala kwa miguu kutoka pande tofauti.
Kwa mujibu wa Makao Makuu ya Arubaini, hadi jana raia milioni 3.32 wa Iran walikuwa wamevuka vivuko vya mpaka wa Iran na kuingia Iraq, na mchakato unaendelea bila matatizo.
Katika Siku ya Arbaeen ya Imam Hussein kila mwaka, mamilioni ya Waislamu kutoka pembe mbalimbali za dunia humiminika Karbala kuzuru kaburi la mjukuu huyo wa Mtume muhammad (saw). Makundi makubwa ya waombolezaji husafiri kwa miguu kuelekea mji huo mtakatifu ili kushiriki katika mkusanyiko mkubwa zaidi wa kila mwaka wa Kiislamu duniani.