IQNA

Rambirambi

Ayatullah Khamenei katika ujumbe baada ya kuuawa shahidi Sinwar: Hamas iko hai na itabakia kuwa hai

16:21 - October 19, 2024
Habari ID: 3479615
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe kufuatia kuuawa shahidi kamanda shujaa wa Mujahidina, Yahya Sinwar, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, HAMAS, na kusisitiza kuwa: "Kama vile safu ya Muqawama (mapambano ya Kiislamu) haikuacha kusonga mbele kwa kuuawa shahidi shakhisia wake mashuhuri, vivyo hivyo haitakoma kwa kuuawa shahidi Sinwar."

Akiyahutubu mataifa ya Kiislamu na vijana mashupavu wa eneo hili katika ujumbe huo wa rambirambi, Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, Sinwar ameungana na masahibu wake waliouawa shahidi.
Huku akimtaja Sinwar kuwa shakhsia mashuhuri wa Muqawama, Ayatullah Khamenei amepongeza azma yake ya kusimama dhidi ya adui katili na kuongeza kuwa, mwanamuqawama huyo alistahiki kufikia kiwango cha mauaji ya shahidi baada ya juhudi zake za kupambana na utawala ghasibu wa Israel.
Ayatullah Khamenei amebainisha kuwa, hakuna shaka kwamba, kumpoteza Sinwar ni uchungu  kwa mrengo wa Muqawama, lakini anasisitiza kuwa Mapambano hayakoma kwa kuuawa viongozi wake.
"Muqawama hautakoma Inshallah. Hamas iko hai na itabakia kuwa hai,” amesisitiza Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Katika ujumbe wake huo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, ameelezwa kuwa, mtu mfano wa Yahya Sinwar ambaye ametumia maisha yake yote katika mapambano dhidi ya adui mporaji na dhalimu, hategemei mwisho wowote ghairi ya kuuawa shahidi.
Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, kuondokewa na kamanda Yahya Sinwar bila shaka ni tukio chungu kwa kambi ya Muqawama, lakini mrengo huo wa Mapambano haukutetereshwa na mauaji ya watu mashuhuri kama vile Sheikh Ahmed Yassin, Fathi Shaghaqi, na Ismail Haniyah, na Muqawama hautasambaratika hata kidogo kwa kifo cha kishahidi cha Sinwar.

3490335

captcha