IQNA

Muqawama

Shahidi Yahya Sinwar alikuwa kamanda aliyepigania Umoja wa Waislamu

23:14 - October 20, 2024
Habari ID: 3479621
IQNA - Mchambuzi wa kisiasa wa Lebanon ameuelezea shahidi Yahya Sinwar kama kamanda wa muqawama wa kupigiwa mfano ambaye alifanya juhudi bila kuchoka katika njia ya umoja wa Kiislamu wa Jihadi.

Sinwar, kiongozi wa harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, yenye makao yake huko Gaza, aliuawa shahidi katika shambulio la kigaidi la wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel katika mji wa Rafah katika Ukanda wa Gaza.
Katika makala moja, mchambuzi wa Lebanon Ahmed Farhat amendika kwamba Sinwar alikuwa mtu wa Jihad ambaye alitumia muda wake mwingi kwenye mstari wa mbele wa Jihadi na licha ya yale ambayo adui alisema, hakujificha kwenye mashimo kama wanavyojificha Wazayuni. Zifuatazo ni nukuu za makala:
Katika ngazi ya kijeshi, Sinwar alipigana kwenye njia ya muqawama kwa ajili ya kuutumikia Uislamu. Aliyachukulia mapambano haya kuwa ni Jihad kwa ajili ya ukombozi wa Palestina na kupigana kwenye njia ya ukweli.
Alijitahidi sana kwa ajili ya ushirikiano na umoja wa Jihadi katika Umma wa Kiislamu. Ndiyo maana uhusiano wake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Hizbullah na makundi mengine ya harakati ya muqawama uliegemezwa kwenye fikra ya umoja.
Alimuandikia barua Katibu Mkuu wa Hizbullah shahidi Sayed Hassan Nasrallah na kusema kwamba moja ya kanuni za Hamas ni Jihad na muqawama na umoja wa Umma wa Kiislamu kukabiliana na mradi wa Kizayuni na kutetea matukufu ya Kiislamu.
Sinwar, pamoja na Ismail Haniya, pia walifungua njia ya ushirikiano na muqawama wa Kiislamu nchini Iraq, Syria na Yemen.
Mashahidi hao wawili waliamini katika haja ya nchi za Kiislamu kukaribiana zaidi na kufanya juhudi za kuwa karibu na harakati za muqawama wa Kiislamu katika eneo.
Katika barua aliyomwandikia Abdul Malik Badreddin al-Houthi, kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen miezi michache iliyopita, Sinwar aliandika kwamba juhudi zinazofanywa na vikosi vya muqawama huko Palestina, Yemen, Lebanon na Iraq zimeongezeka maradufu na kutoa vipigo kwa maadui.
Ushindi ambao Mungu ameahidi utapatikana katika hatua tatu za subira, uthabiti na ushindi. “Na walipo toka kupambana na Jaluti na majeshi yake walisema: Mola wetu Mlezi! Tumiminie subira, na isimamishe imara miguu yetu, na utusaidie tuwashinde watu Makafiri.” (Aya ya 250 ya Surah Al-Baqarah)

Habari zinazohusiana
Kishikizo: Sinwar hamas
captcha