IQNA

Muqawama

Ayatullah Khamenei: Marekani na washirika wake wanakosea kabisa wanapodhani Muqawama umefika ukingoni

21:40 - December 17, 2024
Habari ID: 3479913
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema kuwa Marekani na washirika wake wanakoseka kikamilifu wanapodhani kwamba Muqawama umeishiwa nguvu na umefika ukingoni.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo Jumanne jijini Tehran wakati alipoonana na maelfu ya akinamama na wasichana siku chache kabla ya maadhimisho ya Siku ya Kuzaliwa Bibi Fatimatuz Zahra SA na kuongeza kuwa, matukio ya Syria na jinai za utawala wa Kizayuni na Marekani yasiwafanye maadui hao wadhani kwamba nguvu za Kambi ya Muqawama zimeisha. Watakuwa wamekosea kabisa wakidhani hivyo. 

Amesema: "Utawala wa Kizayuni unataka kuizingira na kuiangamiza Hizbullah ya Lebanon kupitia Syria lakini itakayoangamia ni Israel, si Muqawama wa Lebanon."

Ayatullah Khamenei pia amesisitiza kwamba, roho za viongozi wa Hizbullah na Hamas bado ziko hai na zitaendelea kuwa hai licha ya kwamba wameuliwa shahidi kikatili na utawala wa Kizayuni. 

Amesema: "Miili yao (viongozi wa Hizbullah na HAMAS) inaweza kuwa haipo tena duniani, lakini ... roho na mawazo yao bado yamebaki na njia yao itaendelezwa."

Akigusia pia Muqawama wa kihistoria wa wananchi wa Ghaza mbele ya mashambulizi ya kila siku ya Israel pamoja na ustahimilivu wa Muqawama wa wananchi wa Lebanon na kusisitiza kuwa, Iran itaendelea daima kuwa pamoja na wanamapambano Palestina na Hizbullah na itaendelea kuwaunga mkono na kuwapa msaada wowote ule.

Vilevile amewapongeza wanawake wa Iran kwa kushiriki vilivyo katika nyanja za kisiasa, kimataifa na kisayansi.

Pia amesema kuwa, maadui wanatumia mbinu laini kama vile propaganda na kaulimbiu za uwongo na vishawishi, baada ya kubaini kuwa Mapinduzi ya Kiislamu Iran hayawezi kushindwa kwa njia za mabavu kama vita, mabomu, ukabila na fitna nyinginezo.

.

3491094

Habari zinazohusiana
captcha