Kamal Abu Awn amesema shahidi Sinwar, ambaye aliuawa shahidi mwezi uliopita akiwa katika mapambano na askari wa jeshi la kigaidi la Israel, aliwaheshimu sana wahifadhi Qur'ani na kuwafananisha na wapiganaji wa Brigedi za Al-Qassam, tawi la kijeshi la Hamas.
"Siku zote nilipokutana na na Abu Ibrahim (Yahya Sinwar)," alisema kuwa kabla ya kuwa kiongozi wa Hamas, alikuwa muumini na alilelewa katika misikiti na vikao vya Qur’ani.
Amesema shahidi Sinwar alihimiza uhifadhi wa Qur'ani miongoni mwa wanachama wa Hamas na wengineo.
Mara moja alitoa kitita cha dola 400,000 kwa Hamas, ambapo alitenga nusu ya fedha hizo kwa Al-Qassam na nusu nyingine kwa Kituo cha Dar-Quran, Abu Awn alisema.
Hiyo ndiyo sababu moja wapiganaji wengi wa Hamas unaowaona katika medani ya vita hivi leo wamehifadhi Qur’ani Tukufu, amesema.
Shahidi Yahya Sinwar alizaliwa katika kambi ya wakimbizi huko Khan Yunis, Ukanda wa Gaza, mwaka wa 1962 na alikuwa mpigania ukombozi wa wa Palestina.
Mhitimu wa masomo ya Kiarabu kutoka Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Gaza, alifungwa jela na utawala wa Israel mara kadhaa tangu 1982.
Aliptisha miaka 22 ya maisha yake katika magereza ya kuogofya Israel, wakati huo alijifunza lugha ya Kiebrania na kutafsiri vitabu kadhaa kutoka kwa Kiebrania na Kiingereza hadi Kiarabu.
Pia aliandika idadi ya riwaya, ikiwa ni pamoja na "Mwiba na Carnation" (Iliyochapishwa katika 2004).
Sinwar aliuawa shahidi katika mapambano makali na jeshi la kigaidi la Israel huko Gaza mnamo Oktoba 16, 2024.
4245596