IQNA

Wajumbe wa Jumuiya ya Qur'ani ya Iran watembelea Walebanon waliojeruhiwa

15:43 - October 29, 2024
Habari ID: 3479666
IQNA - Kundi la wanachama wa Jumuiya ya Qur'ani ya Iran wametembelea watu wa Lebanon, ambao wamejeruhiwa katika shambulio la Israel, katika hospitali jijini Tehran.

Ziara hii iliandaliwa na Kamati ya Mashahidi ya Kitengo cha Qur'ani na Etrat ya shirika la Tehran Basij.

Katika ziara hiyo ya saa mbili, maafisa kadhaa wa Qur'ani na watu mashuhuri, akiwemo Rahim Ghorbani, Mohammad Khajavi, na Mohammad Taqi Mirzajani, walikutana na watu waliojeruhiwa.

Walimu wa Qur'ani walisoma aya za Qur'ani Tukufu, ambapo  vijana kadhaa wa Lebanon waliojeruhiwa pia walishiriki kwa qiraa hiyo.

Kama ishara ya nia njema, kila mgonjwa na mfanyakazi wa hospitali alipokea Msahafu na ua.

Mamia ya Walebanon, raia na wanachama wa Hizbullah, walijeruhiwa katika shambulio la kigaidi la Israel dhidi ya vifaa vyao vya mawasiliano vya pager mnamo Septemba 17. Vifaa hivyo vilitegwa mabomu vikiwa viwandani na kulipuka kwa wakati mmoja wakiti vikwai vinatumiwa, na kusababisha mamia ya watu kupoteza maisha au kujeruhiwa kote Lebanon na maeneo ya Syria.

Baadhi ya majeruhi wamehamishiwa Iran kwa matibabu.

3490471

captcha