IQNA

Al-Azhar yalaani mashambulizi ya kigaidi ya Israel huko Lebanon, Gaza

21:45 - September 27, 2024
Habari ID: 3479499
IQNA - Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri kimelaani ukatili wa Israel huko Lebanon na Ukanda wa Gaza.

Katika taarifa yake, Al-Azhar imelaani vikali mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel dhidi ya Lebanon ambayo yamesababisha vifo vya mamia ya raia wakiwemo wanawake na watoto.
Imetoa wito wa mshikamano wa jumuiya ya kimataifa na watu wa Palestina na Lebanon.
Mashambulizi ya utawala wa Israel dhidi ya Lebanon yanaashiria malengo ya jinai ya utawala huo na majaribio yake ya kugeuza Mashariki ya Kati kuwa eneo la vita, ilisema taarifa hiyo.
Baada ya kuharibu Ukanda wa Gaza na kusababisha umwagaji damu huko kwa kuwalenga maelfu ya raia wasio na hatia, utawala huo sasa unalenga kueneza vita katika maeneo mengine, iliongeza.
Al-Azhar ilisikitishwa na kushindwa kwa nchi za dunia kukabiliana na ugaidi wa utawala wa Kizayuni na kusimamisha mauaji ya wanawake na watoto.
 “Je, wana maslahi ya pamoja na utawala huu wa kigaidi? Au dhamiri ya ulimwengu imekufa?” ilijiuliza.
Taarifa hiyo pia imeitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka kukomesha mauaji ya watu wasio na hatia huko Gaza na Lebanon.

3490039

Habari zinazohusiana
captcha