IQNA

Jinai za Israel

Israel yabomoa msikiti wa kale Lebanon

21:57 - October 13, 2024
Habari ID: 3479586
IQNA-Mashambulizi  kinyama ya anga yanayofanywa na  katili la utawala wa Kizayuni wa Israel yameteketeza kikamilifu msikiti wa kale na kubomoa soko kusini mwa Lebanon, katika kile kilichoelezewa kama "uangamizaji wa kila kitu".

Hayo yanajiri huku utawala huo ghasibu ukishadidisha na kupanua mashambulizi yake ya mabomu na makombora katika kila pembe ya nchi hiyo.
Katika shambulizi la karibuni zaidi lililofanywa mapema leo, jeshi la utawala wa Kizayuni limeuteketeza kikamilifu msikiti wa zamani katika kijiji cha Kfar Tibnit kusini mwa Lebanon. Taarifa kamili za idadi ya vifo hazijaweza kupatikana.
Kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Lebanon, shambulio jengine lililofanywa usiku wa kuamkia leo kwenye soko lililoko katika mji Nabatieh kusini mwa nchi hiyo limeua shahidi watu kadhaa. Hata hivyo idadi halisi ya waliofariki na kujeruhiwa bado haijajulikana kutokana na moto mkubwa uliosababishwa na shambulio hilo.
Duru za habari zimeripoti kuwa, Shirika la Msalaba Mwekundu la Lebanon lingali linajaribu kuona "kama kuna walionusurika na kujaribu kuwaondoa waliojeruhiwa" kwenye eneo la shambulio.
Mashuhuda wa shambulio hilo la kinyama lililofanywa na jeshi la utawala wa Kizayuni wameielezea hali ya maafa kuwa ni sawa na maangamizi kamili kwa sababu mitaa yote ya eneo hilo imeteketezwa.
Harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imejibu kwa mashambulizi mengi dhidi ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu kama njia ya kulipiza kisasi utawala huo ghasibu na kuonyesha uungaji mkono kwa Wagaza waliokumbwa na vita.

3490254

Habari zinazohusiana
captcha