IQNA

Muqawama

Majibu ya Iran kwa uchokozi tarajiwa wa Israel yataunda mustakabali mpya

17:45 - October 08, 2024
Habari ID: 3479559
IQNA - Mchambuzi mashuhuri wa Lebanon anasema jinsi Iran inavyojibu kwa shambulio linalowezekana la Israel itaunda mustakabali wa eneo hilo.

Profesa wa chuo kikuu cha Lebanon Talal al-Atrisi amesema leo changamoto kuu ni kukabiliana na uwezekano wa uvamizi wa Israel. Makabiliano hayo yataunda njia na  mustakabali wa eneo, sio tu mustakabali wa mhimili wa muqawama lakini kanda nzima,"

Alitoa kauli hiyo alipokuwa akihutubia tukio la mtandaoni kuhusu matukio ya kikanda wiki hii.

Matamshi hayo yanakuja takriban wiki moja baada ya jeshi la Iran kutekeleza Operesheni ya Ahadi ya Kweli II, inayolenga jeshi la Israel na maeneo ya usalama katika shambulio kubwa la makombora. Tehran imesema operesheni hiyo ni jibu halali kwa jinai za Israel za kumuua kiongozi wa Hizbullah Sayyed Hassan Nasrallah, mkuu wa Hamas Ismail Haniya na kamanda wa IRGC Abbas Nilforoushan.

Utawala wa Israel umedai kuwa utajibu operesheni hiyo. Wakati huo huo Iran imeonya kuwa uchokozi wowote wa Israel utakabiliwa na jibu kali zaidi.

Kwingineko katika hotuba yake, mchambuzi huyo aliashiria kumbukumbu ya Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, iliyoanzishwa na harakati za muqawama wa Palestina katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa ili kukabiliana na miongo kadhaa ya jinai za Israel dhidi ya Wapalestina katika maeneo yote yanayokaliwa kwa mabavu.

Vita vya Israel dhidi ya Gaza vimesababisha vifo vya Wapalestina 42,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, huku takriban watu wote milioni 2.3 wakiwa wakimbizi.

3490185

Habari zinazohusiana
captcha