Qari wa Iran Mehdi Shayegh alitunukiwa tuzo ya kwanza katika kategoria ya qiraa, wakati Hani Sahib Zaman kutoka nchi mwenyeji na Mohamed Ahmed Fathullah kutoka Misri aliibuka wa pili na wa tatu mtawalia.
Katika kategoria ya kuhifadhi Qur'ani nzima, jopo la majaji lilimtangaza Mohamed Sami Subhi Mutawalli kutoka Palestina kuwa mshindi wa zawadi ya kwanza.
Mshindi wa pili alikuwa Imad Mustafa Hassan kutoka Libya na mshindi wa tatu alikwenda kwa Ahmed Jarallah Abdul Rahman kutoka Iraq.
Akizungumza katika hafla hiyo, mkuu wa kamati ya maandalizi Ali Razuqi al-Lami alibainisha kuwa mashindano hayo yalifanyika kwa siku sita kwa msaada wa Waziri Mkuu wa Iraq Mohammed Shia' Al-Sudani.
Ameongeza kuwa wasomaji na wahifadhi Qur'ani kutoka zaidi ya nchi 30 za Kiarabu na Kiislamu walishiriki katika mashindano hayo.
Qari maarufu wa Misri Ahmed Ahmed Nuaina pia alihutubia sherehe hiyo, ambapo amesifu mpangilio mzuri wa shindano hilo.
Mashindano hayo yamefanyika chini ya kaulimbiu ya, “Kutoka Baghdad, Nembo ya Ustaarabu na Uislamu, hadi Gaza, Nembo ya Muqawama, na Lebanoni, Nembo ya Jihadi; Kupitia Qur’ani, Tunapata Ushindi na Uthabiti.”
4248191