IQNA

Harakati za Qur'ani

Kikao cha Qur'ani Katika Haram Tukufu ya Imam Kadhim (AS)

21:02 - November 15, 2024
Habari ID: 3479754
IQNA - Programu ya usomaji wa Qur'ani ilifanyika kwenye kaburi la Imam Kadhim (AS) huko Kadhimiya, kaskazini mwa Baghdad, Iraq Jumatano.

Idadi ya washiriki na wajumbe wa jopo la majaji wa Tuzo ya kwanza ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iraq walishiriki katika program hiyo u ya Qur'ani.
Walijumuisha Ahmed Ahmed Nuaina kutoka Misri, Qassem Raziei, Ali Gholamazad na Mehdi Shayegh kutoka Iran, Omar Abdul Qadir kutoka Nigeria, Muhammad al-Mousawi kutoka Kuwait, Hamuda bin al-Muiz kutoka Tunisia, Muhammad Sami kutoka Palestina na Ahmed Safi kutoka Syria.
Akihutubia katika hafla hiyo, Haidar Hassan al-Shamari, mfawidhi wa haram hiyo tukufu na ambaye pia ni  mkuuu wa Idara ya Wakfu ya Shia nchini Iraq ameashiria umuhimu ambao Wairaqi daima wamekuwa wakiuzingatia kwa Qur'ani na shughuli za Qur'ani.
Amebainisha kuwa katika karne nyingi zilizopita, Iraq imeleta wafasiri wakubwa wa Qur'ani na wanazuoni wa Qur'ani katika ulimwengu wa Kiislamu.
Ameongeza kuwa yeye idara za Awqaf za Shia na Sunni zimekuwa na nafasi kubwa katika maendeleo ya shughuli za Qur'ani katika nchi hiyo ya Kiarabu.
Aidha amepongeza kuandaliwa kwa mashindano hayo ya kimataifa na vituo vya Qur'ani ambavyo vimechangia katika hafla hiyo ya kimataifa.
Tuzo ya kwanza ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iraq ilifanyika katika mji mkuu Baghdad kwa kushirikisha wasomaji na wahifadhi Qur'ani kutoka zaidi ya nchi 30 za Kiarabu na Kiislamu.
Ilihitimishwa katika hafla ya utoaji tuzo siku ya Alhamisi asubuhi.

 

3490689

captcha