IQNA

Muqawama

Hizbullah ilipata ushindi dhidi ya ‘Adui Aliyejidanganya’, yaishukuru Iran

21:07 - November 28, 2024
Habari ID: 3479821
IQNA - Harakati ya muqawama ya Lebanon Hizbullah imesema imepata ushindi dhidi ya utawala wa Kizayuni, na kuongeza kuwa adui Mzayuni alijidanganya na hivyo alishindwa kudhoofisha azma ya Hizbullah.

Hizbullah imeapa kuwa iko tayari kukabiliana na hujuma zaidi zinazoweza kutokea za Israel dhidi ya nchi hiyo, huku ikizingatia makubaliano ya hivi karibuni ya usitishaji vita yaliyofikiwa kati ya utawala huo na harakati hiyo.

Katika taarifa yake siku ya Jumatano, Hizbullah ilionya kuwa imetayarisha zaidi ya njia 300 za ulinzi kusini mwa Mto Litani, na kusema wapiganaji wake, ambao wamesambazwa kila eneo, wako katika kiwango cha juu zaidi cha utayari.

Wakati huo huo, Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imemshukuru Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kutokana na himaya yake na hatua za kidiplomasia za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran za kusimamisha vita nchini Lebanon.

Kufuatia kusitishwa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Lebanon, harakati ya Hizbullah imetoa taarifa ikitoa shukurani zake kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei, na harakati za kidiplomasia na misaada ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa wananchi na serikali ya Lebanon katika kufikiwa usitisha mapigano nchini Lebanon.

Taarifa ya Hizbullah imeelezwa kuwa, wananchi wa Lebanon wanatoka shukrani kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa sababu ya uungaji mkono na himaya yake kamili kwa Muqawama wa Kiislamu katika nyuga zote, na pia safari za mara kwa mara za Waziri wa Mashauri ya Kigeni, Spika wa Bunge na mshauri mkuu wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu mjini Beirut wakati wa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni.

Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Lebanon yalianza kutekelezwa jana Jumatano, Novemba 27, 2024.

Kwa mujibu wa uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa na jeshi la utawala haramu wa Israel ndani ya jamii ya Wazayuni, asilimia 61 miongoni mwao wanaamini kuwa utawala huo haujapata ushindi katika vita dhidi ya Hizbullah ya Lebanon.

3490858

captcha